Friday, December 14, 2018

WIZARA KUMALIZA CHANGAMOTO MAKAO YA TAIFA YA WAZEE SUKAMAHELA SINGIDA

Na Mwandishi Wetu-Manyoni
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii jana ilitoa zawadi ya Sikuu ya Krismasi yenye thamani ya shilingi 280,000 kwa wazee waishio katika Makao ya Taifa ya Wazee Sukamahela Wilayani Manyoni  kama sehemu ya kuenzi mchango wao kwa Taifa.

Akitoa zawadi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto Wizarani hapo Bw. Sebastian Kitiku aliwaambia wazee hao kuwa serikali inathamini mchango wazee katika ujenzi wa Taifa ndio maana imetoa zawadi hiyo kuwaenzi na kuwakumbuka.

Aidha Bw. Kitiku aliongeza kuwa pamoja na zawadi hiyo ya Krismasi Wizara pia inawahakikishia wazee hao kuwa itamaliza changamoto zote zinazowakabili wazee hao ili waweze kuishi katika mazingira safi na salama.

‘’Nawapa nafasi wazee kuongea na sisi ili tuweze kujua changamoto mlizonazo ili Wizara iweze kuwasikiliza na kuzifanyia kazi kwa ajili ya kuweka mazingira rafiki na salama katika makao haya.’’ Aliwaambia Wazee hao Bw. Kitiku.

Aidha moja ya changamoto inayowakabili  Makao hayo ya Wazee Sukamahela ni ukosefu wa nishati ya umeme jambo lilinalosababisha wazee hao kuishi katika mazingira magumu hasa nyakati za usiku hivyo wazee hao kwa pamoja wameiomba Wizara kutatua chanagamoto hiyo.

Wazee kwa nyakati tofauti walisema baadhi ya Nyumba katika Makao hayo zinavuja maji wakati wa mvua hivyo wameiomba Wizara pia kuangalia uwezekano wakukarabati nyaumba hizo ili kuondokana na tatizo hilo ukizingatia kuwa kwasasa mvua za masika zimeanza kunyesha.

Wizara pamoja na mambo mengine imehaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo ili wazee hao waweze kuishi katika mazingira safi na salama kwa kuwa serikali inawathamini, kuwapenda na kutambua mchango wao hususani mchango wao katika  maendeleo ya Taifa.
 Baadhi ya Wazee pamoja na Watumishi wa Makao ya Wazee Sukamahela wakiwa tayari kupokea zawadi ya Sikuu ya Krismas kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku wa pili kulia mara baada ya kuwasili katika Makao hayo jana.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akikabidhi zawadi ya Siku Kuu ya Krismas kwa mwakilishi wazee waishio katika Makao ya Wazee waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyoko nje kidogo ya mji wa Manyoni jana.
 Baadhi ya Wazee waishio katika  Makao ya Wazee Sukamahela wakijipatia kinywaji mara baada kupokea zawadi ya Sikuu ya Krismas kutoka kwa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku akiongea na  Wazee waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyoko nje kidogo ya mji wa Manyoni jana.

No comments: