Thursday, December 6, 2018

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018 Kufungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano  ya Taifa ya Baseball.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Japan Nchini,    Shinichi Goto wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya  Taifa ya Baseball, kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipofungua kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindu Mshindano ya Taifa ya Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkwe wa Jackie Robinson, Muasisi wa Mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson (katikati) na Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro David Robinson   (kulia) wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya  Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kiwanja Kipya wa Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball  kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto.  Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira huku Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto  (kushoto) akijiandaa kuuzuia wakati Waziri Mkuu alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmoja wa wadhamini wa Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball, Dkt. Kazusue Konoike wakati alipofungua kiwanja hicho na  Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es slaam, Desemba 6, 2018. Katikati ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini. Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam. Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo  UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.

Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.

Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.

Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususan kwa vijana.

“Pia naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa Baseball.”

Amesema jitihada hizo zitaufanya mchezo wa baseball kuwa ni mmoja wa mchezo huo kukua kwa kasi na unachezwa kuanzia ngazi za shule ya msingi na sekondari.

“Nina hakika baada ya hapo Tanzania itaweza kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimaifaifa na hasa yale ya Olimpiki ya Tokyo Japan 2020.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza uwanja huo ulindwe na utunzwe ipasavyo ili utumike katika mashindano ya ndani na nje ili uwe sehemu ya kuitangaza nchi.

Awali, Balozi wa Japan nchini, Balozi Shinichi Goto alisema nchini Japan mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na kujiamini.

Alisema anatarajia kwamba mashindano ya mchezo huo yatakuwa endelevu nchini na wachezaji watacheza vizuri kutokana na uwepo wa uwanja mzuri.

Balozi huyo alisema mchezo huo unafundishwa na walimu wa Kijapani katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments: