Thursday, December 6, 2018

BENKI YA UBA YABORESHA HUDUMA ZA KIMTANDAO KWA KUZINDUA MAGIC BANKING


Ikiwa ni jitahada za kuendelea kuwa benki bora Barani Afrika kwa huduma za simu za mkononi na kuendelea kuendana na jinsi mtandao unapokuwa haraka na kuwa na bidhaa na huduma zilizo bora kabisa, benki ya UBA Tanzania leo imetangaza kuzindua huduma nyingine bora ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70# kwa hapa Tanzania.

Huduma hii ya Magic Banking itamfanya mteja kwa kutumia simu yake ya mkononi kuweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hii ya Magic Banking, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Huduma za Kimtandao UBA Bank Tanzania Asupya Nalingigwa alisema kuwa mbali na huduma ya Magic Banking kufanya kazi kwenye simu aina yeyote ile lakini huduma hii ni salama, ya haraka na nafuu na mteja haitaji kuwa na salio ili kufanya miamala. ‘Huduma ya Magic Banking inamfanya mteja kuweza kufanya miamala ya hadi TZS 1 milioni kwa siku kwa kutumia UBA Secure Pass ambayo inaongeza usalama kwa mtumiaji,’ alisema Nalingigwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji UBA Tanzania Usman Isiaka alisema kuwa huduma ya Magic Banking itamfanya kila Mtanzania mwenye simu iliyosajiliwa kufungua akaunti papo hapo. ‘Mteja anayetumia simu ya mkononi bila kujali anatumia mtandao ngani wa simu anaweza kufungua akaunti na sisi kwa kupiga *150*70# bila gharama yeyote, alisema Isiaka huku akiongeza kuwa kuzinduliwa kwa huduma hii ya Magic Banking ni moja ya lengo ya benki ya UBA kuweza kuwafikia mamilioni ya wananchi ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki kwa kuwaletea huduma ambazo ni rahisi, nafuu na za haraka zinazoendana na teknolojia. Vile vile tumelenga kufikisha huduma rahisi za kifedha kwa wananchi ili kuendana na matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), aliongeza Isiaka.

Isiaka aliongeza kuwa benki ya UBA Tanzania imedhamiria kuboresha huduma za kifedha za kuzindua bidhaa na huduma zenye ubunifu ili kuweza kuwafikia wananchi wengi kwa rahisi ya teknolojia. Ili kuweza kufanikisha yote haya tumewekeza rasimali nyingi na tuna uhakika tutaweza kuwafikia walengwa wetu, alisema AIsiaka.

Uzinduzi wa Magic Banking umeenda sambasamba na kuzindua UBA Mobile banking App ya benki hiyo ambayo mteja anaweza kupakua kwa kupitia App Store na Play Store kwa watumiaji wa simu aina ya iPhone na Android. App hiyo itamuwezesha mteja kuweza kulipia huduma mbali mbali, kuangalia salio, kuomba cheque pamoja na kufanya miamala nyingine ya kibenki kwa kutumia simu zao za mkononi.

Benki ya UBA Afrika imekuwa ikiongoza kwa huduma mbali mbali za kimtandao kwenye masoko yake ambayo yapo kwenye nchi 20 Barani Afrika. Kwa kutambua uwezo wake wa kutumia teknojia kwenye huduma za kifedha, benki ya UBA iliweza kushinda tuzo ya Best Digital Bank tuzo ambazo zilitolewa na Euromoney.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akizungumza waandishi wa habari, Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya benki huduma ya kutumia simu za mkononi ya UBA Magic ambayo inapatikana kwa kupiga *150*70#. Kushoto ni Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya UBA Tanzania, Usman Isiaka akimuelekeza Meneja wa Mifumo ya Malipo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Thomas Mongella jinsi ya kufungua akaunti kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa kuzindua huduma ya UBA Magic Banking ambayo mteja anaweza kufungua akaunti mpya, kuhamisha fedha, kununua muda wa maongezi, kulipia huduma mbali mbali kama vile Dawasco, kuangalia salio pamoja na huduma nyingine za kibenki kwa kupiga *150*70# bila malipo yoyote.

No comments: