Thursday, December 6, 2018

HARMONIZE ATOA PARANAWE YA KUFUNGIA MWAKA WA 2018

Na Baba Faisal

MWENAMUZIKI maarufu kwenye muziki wa kizazi kipya ambaye anafanya kazi zake chini ya Lebo ya WCB Rajab Abdul Kahali a.k.a

Harmonize ameamua kuachia wimbo wake mpya wa Paranawe ambao tayari umeanza kuwa gumzo kwenye vituo mbalimbali vya redio pamoja na mitandao ya kijamii.

Unajua kwanini wimbo huo umeanza kuwa gumzo ?Ukweli ni kwamba licha ya wimbo huo kuwa una siku mbili tangu kuachiwa rasmi na msanii huyo umekuwa gumzo kwasababu Harmonize kupitia wimbo huo amethibitisha yeye ni moja kati ya wasanii bora kutokana na aina ya staili yake anayotumia katika kuimba na nyimbo zake.

Kikubwa ambacho kimeongeza ladha ya wimbo wa Paranawe ni pale ambapo ameamua kumshirikisha Rayvany ambaye kwa hakika sauti yake imefanikiwa kupenya kwenye masikio ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania.Hivyo Harmonize a.k.a Konde Boy ameamua kumpa nafasi Rayvany katika wimbo huo.

Ni jana tu ndio Harmonize ameachia wimbo huo ambao tayari umeshika kasi mtaani.Kama unavyojua tena kwenye bodaboda huko mtaani tayari wameshaweka kwenye flash zao na kilichobaki wanasikiliza mdundo huo wa Paranawe kama sehemu ya kuwa na watu wa kwanza kuusikiliza.

"Kwa mwaka huu ndio wimbo wangu wa kufunga mwaka, sitatoa nyimbo nyingine mpya hadi mwakani,"amesema Harmoze wakati anazungumzia wimbo huo kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijami huku akielezea namna ambavyo Rayvvan ameonesha umahiri wa hali ya juu. Msanii huyo hakusita kumwagia sifa Rayvvany a.k.a Vann Boy.

Hata hivyo Vann Boy naye hakusita kumuelezea Harmonize kutokana na wimbo wake huo ambapo ametumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii kumsifu kwa namna ambavyo amefanya kazi kubwa kuhakikisha anatoa ngoma iliyo bora ya kufungia mwaka.Wakati wimbo huo ukiwa ndio kwanza umetoka, kitendo cha Harmonize kumshirikisha Rayvvany kunathibitisha wawili hao kuwa

wamoja na mambo yao ni motooo.Kwa kukumbusha tu za nyuma kulikuwa na mjadala kwenye vijiwe vya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kuwa wawili hao haziivi lakini wamethibitisha yaliyokuwa yanasemwa hayana ukweli.

No comments: