Sunday, December 9, 2018

TAASISI YA USTAWI WA JAMII WANYAKUA TUZO ZA NBAA KWA MARA YA TATU

          Na.Khadija seif,globu ya jamii.

BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) watoa Tuzo kwa Taasisi,Makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 Bunju jijini Dar es salaam.

Akipokea Tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Athuman Senzota amesema ni kwa Mara ya tatu wananyakua Tuzo hiyo ambapo vilikua vyuo viwili Kwenye kinyang'anyiro cha Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na Taasisi ya ustawi kuwa washindi wa pili huku nafasi ya kwanza kushika chuo cha Mzumbe.

Aidha,Senzota ameeleza kuwa Tuzo hiyo waliyoipata inaonyesha jinsi gani Taasisi yao ya ustawi wa jamii ni waadilifu na wachapakazi wa hali ya juu katika kutunza na kutumia pesa za Umma Kikamilifu kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha 2018.

Hata hivyo amefafanua kuwa Waliweza kufikia viwango ambavo viliwawezesha kushinda Tuzo ambapo ili uweze kushinda Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi ilizingatia viwango vya uwasilishaji kufikia 75% ya Mapato kwa mwaka wa fedha 2018 .

Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Dr.Zena Mabeyo amesema TAASISI ya ustawi wa jamii imewatunuku vyeti wahitimu 1387 katika mahafali ya (42) ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada ,stashahada na shahada ya Ustawi wa jamii katika gani ya mahusiano kazini, menejimenti ya rasilimali watu na Mahusiano kazini hii inaonyesha dhahiri kuwa Taaluma inakua kwa kasi na huku tukiendelea kuzalisha wataalam hasa Afisa ustawi kwani bado ni hitajika katika kila sekta hapa nchini.

"Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla "alisema Mabeyo.

Vilevile ametoa rai kwa Taasisi,Mashirika na Makampuni yaliyofanya Tuzo hizo waendelee kufanya kazi kwa bidii,uwajibikaji madhubuti kwa lengo la kuongeza pato la Taifa na ili kufikia uchumi wa kati.
 Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii  Dr. Zena Mabeyo  akipokea Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha katika nafasi ya Taasisi ya elimu ya juu na Vyuo vikuu  zilizoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) kwa mwaka 2018 jijini Dar es salaam
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii CPA Athuman Senzota akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha kwa mwaka 2018

No comments: