Sunday, December 9, 2018

Equinor kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi wao waliowafadhili.

Equinor Tanzania inaona fahari kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi kumi na tatu miongoni mwa wanafunzi wake wengi inaowafadhili ambao wamekuwa wakichukua masomo ya shahada- ya pili (Uzamili) katika Geoscience and Engineering.

Wanafunzi wanaohitimu wamekuwa wakifadhiliwa chini ya programu ya ufadhili wa Equinor Tanzania unaojulikana kama Angola Tanzania Higher Education (ANTHEI). Programu hii ya ufadhili ya ANTHEI kutoka kwa Equinor ni programu ambayo inatoa ufadhili kamili kwa hadi kufikia wanafunzi kumi kila mwaka kusomea shahada ya pili katika masomo ya (Utafiti wa Petroli) Petroleum Geoscience na Uhandisi wa Petroli (Petroleum Engineering) katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Norway (Norwegian University of Science and Technology) (NTNU) kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Da es salaam (UDSM).
 
 Programu hii imeandaliwa kwa namna kwamba mwanafunzi atatumia mwaka mmoja nchini Norway na kukamilisha mwaka wa mwisho wa masomo ya shahada ya pili katika chuo cha UDSM. Kwa mujibu wa hati ya makubaliano iliyosainiwa na Equinor, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na NTNU mpango huu wa udhamini chini ya Equinor ulianza mwaka 2012 na utaendelea mpaka 2019.

 Jumla ya wahandisi wa Petroli wapatao 42 (Wahandisi wa Uzalishaji, Uhifadhi na wahandisi wa Uchimbaji) wahandisi 16 wa Utafiti wa Petrioli (Geology, Petrophysicis na Geophysics) na wahandisi 6 wa usimamizi wa miradi wameshasajiliwa mpaka sasa.

Akiongea katika sherehe za mahafali Maneja Mkaazi wa Equinor nchini Dr. Mette Halvorsen Ottoy, amesema, “Equinor inaona fahari kufanya kazi kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali katika kuweza kufikia lengo la kujenga uwezo ambalo ni kusudio katika kuendeleza sekta ya gesi na mafuta nchini Tanzania. Ni lengo letu kuona Watanzania wanapata mafunzo na wanavigezo vya kushiriki katika kuchangia katika ukuaji wa sekta hii moja kwa moja au vinginevyo”.

Equinor inatilia mkazo sana katika uendelevu katika shughuli zake zote za uendeshaji duniani kote. Mwelekeo wa Equinor katika uendelevu una maana kuwa, tunachangia katika maendeleo endelevu kupitia shughuli zetu za msingi katika maeneo tunakofanya kazi, aliingeza Dr. Mette.

Kupitia programu za kujenga uwezo pia Equinor imejenga ushirikiano na Vyuo mbalimbali kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi kama vile programu za shahada ya pili (uzamili) katika fedha na utunzaji wa hesabu katika mafuta na gesi ( Master program in Finance and Accounting in Oil and Gas) (MFA-OG) ambayo imeanzishwa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Biashara cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (University of Dar Es Salaam Business School (UDBS) na Chuo kikuu cha Stavanger (University of Stavanger) mwaka huu wanafunzi 25 wamehitimu wakiwa na shahada za uzamili katika Fedha na Utunzaji wa Hesabu katika mafuta na gesi ambapo 10 kati yao walikuwa wamepata ufadhili kamili kutoka Equinor. 
 
Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pia kimesaidiwa kwa kupatiwa msaada wa kiufundi kutoka Chuo kikuu cha Barcelona kuandaa program ya shahada ya uzamili ya sayansi katika petroleum Geoscience kwa msaada wa Analog Modeling Labaratory iliyotolewa na Equinor. 
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen akizungumza jana na  waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo. 
Mhitimu, Bertha Ngereja akitoa shukurani zake kwa niaba ya wenzake kwa wafadhili Equinor Tanzania, ANTHEI, UDSM na NTNU kwa kuwawezesha kupata shahada ya pili ya masomo mbalimbali yanayohusu Mafuta na Gesi. Sherehe za mahafali zilifanyika jana kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dr. Mette H. Ottoy akizungumza jana na  waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo.
Mhitimu, Masolwa Kasongi akipokea cheti cha kuhitimu shahada ya pili ya Geoscience and Engineering jana kwenye sherehe ya mahafali zilizofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

No comments: