Sunday, December 9, 2018

MBUNGE MAVUNDE AZINDUA TAASISI YA WASANII DODOMA,AKABIDHI OFISI NA STUDIO

Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde jana amezindua rasmi Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma.Uzinduzi huo umefanyika leo katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road,Dodoma kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Dodoma.Ofisi hizo na studio.Zitatumiwa na Wasanii wote kupitia umoja wa na Vilabu vya wasanii.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Mavunde amewataka wasanii wa Dodoma kuwa na UPENDO,MSHIKAMANO na UMOJA ili kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Patrobas Katambi amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna anavyowatumikia wana DODOMA na kuahidi kushirikiana nae kuwasaidia Vijana wakiwemo wasanii ili wapige hatua zaidi katika mafanikio ya kwenye sanaa.
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini,Mh Anthony Mavunde pamoja na MKuuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi wakiwa samamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitumbuiza jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kupiga ngoma kwenye moja ya kikundi cha ngoma za asili kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kucheza muziki jukwaani sambamba na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road

No comments: