Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba katika ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini leo Desemba 06, 2018 ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba 07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Dawati la Jinsia katika Jeshi la Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila akichangia jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza yatakayofanyika Desemba 07, 2018.
Meneja Huduma na Mikopo Binafsi kutoka Benki ya NMB Bw. Emmanuel Mahodaga akitoa mada kuhusu huduma za NMB hasa kwa watumishi wa Umma. NMB ni mmoja wa wadhamini wa shughuli za Uzinduzi wa Dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 07 Desemba, 2018 katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Tike Mwambipile akichangia mada katika mafunzo kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo wa Magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Bwalo Kuu la Magereza ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza utakaofanyika Desemba 07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo kuhusu mambo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka Magereza yote nchini yanayofanyika katika Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi hilo. Uzinduzi huo utafanyika Desemba 07, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Mtoa Mada kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Mapunda John ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati la Jinsia kutoka Magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa kike kutoka magereza mabalimbali hapa nchini ambao ni waratibu wa Dawati la Jinsia waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza waliohudhuria mafunzo kuhusu Dawati la Jinsia yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Magereza Ukonga, Dar es Salaam.
Baadhi ya watoa mada na wafadhili wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati waliokaa) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Dawati la Jinsia kwa Waratibu na Watendaji wa Dawati hilo kutoka magereza yote nchini yaliyofanyika leo Desemba 06, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Pwani ACP Rehema Songelaeli, Mratibu wa Dawati la Jinsia Makao Makuu ya Magereza SACP Betha Minde na Mwenyekiti waTaifa wa Dawati la Jinsia ndani ya Magereza Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila. Kulia ni Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Morogoro ACP Elizaberth Mbezi, Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi ACP Josephine Semwenda na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam SACP Julius Ntambala. (Picha zote na Jeshi la Magereza)
No comments:
Post a Comment