Wednesday, November 28, 2018

ZAIDI YA WANANCHI 500 BUTIAMA WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA YA KINYWA CHA MENO.

Na Frankius Cleophace Mara.

Zaidi ya wananchi wanao kadiliwa kufikia miatano wamejitokeza kupata huduma ya kinywa na meno katika wilaya ya Butiama mkoani Mara kupitia huduma ya Madkatari Bingwa wa Afya ya Kinywa na meno.

Imelezwa kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wemekuwa Wakiungua ugonjwa wa kinywa na meno jambo ambalo linahatarisha maisha yao ambapo pia Tatizo Sugu la fizi hupelekea kutokea kwa Magonjwa mengine ikiwemo Magonjwa ya moyo na sukari.

Hayo yamebainishwa na Rais wa chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania Daktari Ambege Jack Mwakatobe wakati wa utoaji huduma hiyo kwa wananchi wa Wilaya ya Butiama ,Mwitongo mkoani Mara

Daktari Mwakatobe amesema kuwa uwepo watatizo hilo ndio chanzo kikubwa cha kupelekea kutoa huduma hiyo ambapo waliamua kufanyia wilayani Butiama ikiwa lengo nikumuenzi Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa watalamu wa Tatizo hilo katika hospitali za wilalaya.

“Tulishwahi kuja awali tukagundua kuwa kuna uhitaji mkubwa sana wa kutoa hudma ya matatizo ya Fizi ndio maana tumeamua kuja kutoa huduma hii ambapo novemba 28 tunamkutano wetu wa madaktari Bingwa.” Alisema Mwakatobe.

Pia alisema kwa Mujibu wa Utafiti wa uliofanywa na hospitali ya muhimbili ni mika 10 mfululizo Asilimia 80 ya watu wazima wamekuwa na matatizo ya kinywa na meno huku watoto kuanzia miaka 12 nao wakikumbwa na matatizo hayo ya kinywa na meno hivyo kuepelekea kushindwa kutimiza ndoto zao za masomo.

Serikali ya wilaya ya Butiama kupitia mkuu wake Wawilaya Bi.Annarose Nyamubi Alipongeza ujio wa madkatari hao huku akiwataka wananchi kutumia Fursa zinazojitokeza kutoka kwa madaktr Bingwa ,ambapo alisema wanauhitaji mkubwa wa watoa huduma kutokana na wingi wawananchi wenye matatizo hayo.

Costanzia Malyabibi nimmmoja ya wananchi walipata nafasi ya kuhudumiwa ambapo wanaipongeza serikali kwa kuwajali wananchi wake kwa kuwasogezea huduma huku wakiomba zinapotokea fursa kama hizo basi zitoke kwa mda mrefu ili kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na upatikanaji wa huduma hiyo ambayo imekuwa ikileta matatizo mengi.

Chama cha Madkatari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania kinatarajiwa kufanya mkutano wake katika manispaa ya Musoma Novemba 28 huku Mgeni Rasimi wa Ufunguzi wa mkutano huo akitarajiwa kuwa waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu.
Mkuu wa wilaya ya Butiama Anarose Nyamubi akiongea na baadhi ya waginjwa wa maeneo katika eneo la madaktari bingwa wa Kinywa na meno wanapotoa huduma.
Madaktari bingwa wa kinywa na Meno wakiendelea na matibabu ikiwemo kungoa Meno katika eneo la Mwitongo Wilayani Butiama Mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wakipatiwa elimu jinsia ya kutunza vinywa na Meno.
Wanafunzi wa Sekondari wa Sekondari wakipatiwa elimu ya kutunza Kinywa na Meno.

No comments: