Wednesday, November 28, 2018

MZAZI AFURAHI KUUAWA KWA MWANAE.

JOSEPH MPANGALA,MTWARA.

Mwanamke Mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ndilikuli Matupa Mkazi wa kijiji cha Mkangaula Kata ya Namalenga wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ameshukuru wananchii wenye hasira Kali kwa Kumchoma Moto Kijana wake Abdallah Hussein Mahona kwa Tuhuma za Kuhusika na matukio Kadhaa ya Ukabaji,Unyang'anyi na Mauaji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 12 asubuh mwanzoni mwa wiki hii ambapo marehemu alihusishwa na kuwajeruhi watu wawili ndipo wananchi wenye hasira wakamtafuta na kumchoma moto mpaka kifo chake.

Akiongea katika eneo la Tukio ambalo Marehem Abdallah Hussein amechomwa mama yake Mzazi Bi Ndilikuli Matupa anasema alilazimika kulala nyumba za stareh {Disco}ili kuepuka kuuawa na Mwanae ambapo mara kadhaa amekuwa akimtishia Kumuua.

“Sina Masikitiko yoyoyote Mzazi Mimi,Nimepona kwa chukuchuku kila siku Mwenye disko mtu mkubwa kama Mimi nilikuwa nawaacha wajukuu wangu Mmoja wa Marehem Mmoja wa kaka yake mimi nakwenda kwenye disco ilihali mimi sio mtu wa disco yaan kukimbia Kifo”alisema Bi Ndilikuli Matupa ambaye ni Mama wa marehem.

Hata Hivyo Bi Ndilikuli ameongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa Marehem mwanae Kumtishia kumuua kwa kumtuhumu kuwa ni Mchawi kutokana na Mtoto wa Marehemu Kuumwa kwa kipindi cha Muda Mfupi.

“Kwanza kifo Cha kwanza kabisa nilitaka kuuwawa kutokana na Mtoto wake Yupo hapa Mohamed Kuumwa tu Mudy nikataka kuuwawa nikasema huyu anaumwa tu sio kwa kumroga mimi nimroge mimi kwa sababu gani”Alisema Mama wa Mzazi wa Marehem.

Mnape Mohamed Mnape ni Mmoja wa ndugu wa Marehem wanaoishi kijijini hapo anasema ndugu yake alikuwa akizulumu watu na mara nyingi alikuwa akimpiga mama yake Mzazi na mara nyingi alikuwa akitembea na Panga mkononi.

“Huyu mimi ni ndugu yangu na matukio yake nayafaham tokea siku za nyuma na hata juzi nilikuwa naye kwanza alifikia kuwa katili kuwazulumu watu mpaka imefikia hatua ya kumpiga mama wakati akitoka kwenye sherehe”amesema Mnape ambaye ni Ndugu wa Marehem.

Lakini naye Mtendaji wa kata ya Namalenga ambapo ndipo marehema alikuwa akiishi Sijaona Binamu anasema pindi aliporipoti kazini mwezi wa saba mwaka 2016 taarifa ya kwanza ya kiuhalifu ilimtuhumu marehema Abdallah kwa kuua mwanzafunzi wa kudato cha kwanza mwaka 2010.

“Niliporipoti mwaka 2006 taarifa ya kwanza niliyopewa ilikuwa ni Marehem Kutuhumiwa kumuua mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2010 na akatoweka hapa kijijini kwa muda wa miaka mitatu lakini baada ya miaka mitatu akaanza kujionesha kidogo kidogo mpaka mazingira alipoona ni rafiki kwake ndio akaendelea na matukio Mengine”alisema Sijaona Binamu.

Hata Hivyo jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara bado linaendelea na Uchunguzi ili kubaini sababu halisi ya Kifo hicho.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga tarafa ya Lulindi wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamekusanyika kutazama mwili wa marehem Abdallah Hussein Mahona aliyechomwa Moto kwa Tuhuma za Ukabaji na Unyang’anyi.
Mabaki ya mwili wa marehem Abdallah Hussein mahona ambaye ameuwawa kwa kuchomwa moto na wananchii wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuwa kibaka ambapo wananchii wa kijiji hicho walikusanyika kwa ajili ya Kuutazama.
 
No comments: