Thursday, November 29, 2018

Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu

 Mshehereshaji George Mulamula (kushoto) wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 akiitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dkt. Phillip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ambao ni wafadhili wa ripoti hiyo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya wakisikiliza salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya akitoa salamu NBS kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa nne kulia) akikata utepe kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya (kulia) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa tatu kulia).
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mtafiti mshiriki mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),Prof Samuel Wangwe akiwasilisha ripoti kuhusu hali ya ustawi wa jamii Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akizungumzia masuala ya kisera katika mabadiliko ya kiuchumi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mtaalam na Mratibu wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akizungumzia utengenezaji wa ripoti hizo kwa siku za usoni ambapo ameahidi kufikisha ripoti hizo katika vyuo mbalimbali 
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Washiriki wakiuliza maswali wakati wa kujadili maeneo mbalimbali ya wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya akipitia nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
 Washiriki wakipitia nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara bada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali bara na visiwani, ESRF, Umoja wa Mataifa pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma walioshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini Tanzania ya Mwaka 2017 (THDR) inayozungumzia  “Sera ya Kijamii Katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi”, ina mchango mkubwa katika kuchambua masuala yanayohusu maendeleo ya binadamu na nafasi yake katika uandaaji wa mipango ya maendeleo, utengenezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa uzinduzi wa ripoiti hiyo mjini Dodoma jana.

“Kwa mtazamo wangu, dhana hii ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi sio tu kwamba ni dhana sahihi bali pia inaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 – 2020/21.’ Alisema Dk. Mpango .

Aidha, alisema dhana ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi ni dhana ambayo imekuwa ikizingatiwa katika mipango ya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja pamoja na miongozo ya uandaaji wa bajeti za serikali.

Dk. Mpango alisisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi, kutokuacha mtu yeyote nyuma katika mchakato wa maendeleo na kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya uchumi, serikali ya Tanzania imetoa umuhimu mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ili kuinua hali za watu wake.Waziri Mpango alisema kwamba sekta ya afya, elimu na miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ni sehemu ya juhudi zinazofanya kuwezesha uchumi jumuishi.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwamba kutokana na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika utoaji wa huduma za kijamii na kuinua maisha ya watu wake, kiwango wastani wa umri wa Mtanzania umeongezeka kutoka miaka 62.2 mwaka 2013 hadi miaka 64.4 mwaka 2017.

Alisema ni matazamio ya Serikali ni kuendelea kuboresha huduma za jamii ili kwamba kiwango cha wastani wa maisha ya Mtanzania yawe ni miaka 66.1 ifikapo mwaka 2020.    Alisema ni mtazamo wa serikali ya Tanzania kutoa huduma za kijamii kama afya, elimu na maji kwa umuhumi sawa na uwekezaji katika misingi ya uchumi kama ujenzi wa reli na barabara kwani pande hizi mbili zinategemeana na kusaidiana katika mchakato wa ujenzi wa uchumi wa kisasa.   

Akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 Mkurugendaji Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida alisema kwamba ripoti hiyo ni ya pili kitaifa nchini Tanzania.
Aidha alisema kwamba Mada kuu ya ripoti ya mwaka ya “Sera ya Kijamii katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi” ilichaguliwa makusudi ili kuendeleza dhana zilizoibuliwa na Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya mwaka 2014, ya umuhimu wa mageuzi ya kiuchumi ambayo Tanzania imedhamiria kuyafanya kama inavyoelekezwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 iliyobeba mada ya “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu dhana kuu ilikuwa ni mageuzi ya kiuchumi yalete maendeleo ya binadamu.

“Kiukweli mchakato wa mageuzi ni lazima uende sambamba na upatikanaji wa ajira, ongezeko la kipato na utoaji wa huduma za jamii. Hivyo, Ripoti hii ya mwaka 2017 imelenga kuendeleza fikra za ripoti iliyotangulia katika kuchambua nafasi ya sera ya kijamii na utoaji wa huduma za kijamii katika mchakato endelevu wa mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania, “ alisema
Miongoni kwa matokeo muhimu katika utafiti uliofanyika katika ripoti hii ni pamoja na kuonesha kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya binadamu, maendeleo ambayo yanathibitishwa na kuongezeka kwa alama za Kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kutoka 0.371 mwaka 1985 hadi 0.531 kwa mwaka 2015 ambalo ni ongezeko la asilimia 43.1 kwa kipindi cha miaka 30 (UNDP 2016).

Kwa kuzingatia alama za mwaka 2015, Tanzania imepanda daraja ambalo ni zaidi ya wastani wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo ni 0.518.
Aidha ripoti hii imeonesha pia kwamba kiwango cha umaskini kwa kutumia kipimo cha vigezo mbali mbali yaani MPI umepungua toka kiwango cha asilimia 64.0 mwaka 2010  hadi asilimia 47.4  mwaka 2015. Kwa mujibu wa utafiti huu, mafanikio haya yamesababishwa na kuboreka kwa maisha ya Mtanzania katika maeneo mbali mbali hususan elimu na afya pamoja na ongezeko kubwa la upatikaji wa huduma ya umeme miongoni mwa wananchi.

Pamoja na mafanikio haya, ripoti hii imeonesha pia kwamba Tanzania bado ina safari ndefu kuelekea katika viwango vya juu vya maendeleo ya binadamu yanayokusudiwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa.
Mchakato wa uandaaji wa ripoti hii ulioratibiwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na kikosi kazi cha zaidi ya wataalamu thelathini (30) toka taasisi mbali mbali nchini ina sura nne pamoja na viambatanisho vya takwimu.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ameelezea kufurahishwa kwake na ripoti hiyo na kusema inaonesha juhudi za serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa lengo la kubadilisha hali ya wananchi wake na kuwa bora zaidi.

Alisema ripoti hiyo inaonesha njia inayochukuliwa na Tanzania kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wake kupitia mipango mbalimbali ya kukabiliana na umaskini ikiwamo MKUZA na FYDP.

Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ikishirikiana Wakala wa taifa wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na kitivo cha uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP .

Ripoti hii inapatikana kwenye anuani zifuatazo
http://www.thdr.or.tz/
http://www.esrf.or.tz/
http://www.tz.undp.org/

No comments: