Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Florida Sianga (kushoto), akiwaelekeza Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Naliendele iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Abdallah Njee (katikati) pamoja na Mtunza Dawa wa Zahanati hiyo, Pili Makota (kulia), jana, mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini jinsi ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD. Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Mtwara, Larisa Manyahi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko akizungumzia upatikanaji wa dawa katika mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Joseph Kisala, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika halmashauri hiyo.
Jengo la Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Rwelu
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Shadida Rashidi (katikati), akimuonesha moja ya kopo lenye dawa Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga. Kulia ni Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Ligula Mtwara, Boniface Magige.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Edwin Manyama akizungumzia upatikaji wa dawa.
Mkazi wa Kijiji cha Rwelu, Lukia Matipa (kushoto), akizungumzia jinsi anavyopata dawa anapokwenda kutibiwa katika Zahanati ya Rwelu.
Mjumbe wa Kamati ya Afya wa Kijiji cha Rwelu, Salum Chimbiaka, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo.
Mtunza Dawa katika Zahanati ya Naliendele, Pili Makota akielezea namna wanavyo nunua dawa kutoka MSD. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abdallah Njee.
Mkazi wa Kijiji cha Naliendele,Hamisi Chikambu akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati ya kijiji chao. Kushoto ni mtoto wake Kauthari aliyempeleka kutibiwa kwenye zahanati hiyo.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Florida Sianga (kulia), akimuelekeza, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Likombe, Nuru Namkuna, mfumo maalum wa kieletroniki/kidigitali unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini jinsi ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake.
Mkazi wa Mtwara mjini, Furaha Masanja akizungumzia huduma nzuri alizopata wakati alipofikishwa kujifungua katika Kituo cha Afya cha Likombe.
Na Dotto Mwaibale, Mtwara
IMEELEZWA kuwa upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani Mtwara ni asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa chini ya asilimia 40.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko, wakati akizungumza na waandishi wa habari na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao wapo mkoani humo kuwatembea wateja wao na kujua changamoto walizonazo ili kuzifanyia maboresho.
"Hivi sasa hali ya upatikaji wa dawa katika mkoa wetu ni nzuri tumefikia asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo tulikuwa chini ya asilimia 40" alisema
Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Mtwara Ligula, Boniface Magige alisema changamoto kubwa waliyonayo ni ukusanyaji wa fedha vituoni baada ya kupelekewa dawa pamoja na kada ya wafamasia kuwa wachache.
Katika hatua nyingine MSD imetambulisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wateja wake, ambazo ni pamoja na taarifa za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD.
Taarifa hizo zinapatikana kwenye mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.
Akizungumzia mfumo huo Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga alisema kupitia mfumo huu, MSD imedhamiria kuongeza ufanisi katika kuhudumia vituo vya kutolea hudumaza afya nchini ili kuhakikisha adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi inatimizwa kwa vitendo.
“Mfumo huu unalenga kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wataarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vinavyotolewa na MSD kwa vituo vya kutolea huduma za afyanchini, kwa kuviwezesha vituo hivi kupata taarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati popote walipo nchini hata kupitia simu zao za mkononi” alisema, Sianga.
Aliongeza kuwa mfumo huu, utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za upatikanaji wa dawa ghalani (stock status) iliiwerahisi kwao kuagiza mahitajiyao MSD kulingana na matakwayaokwawakatihusikahata pale wanapokuwa na mahitajiya dharura.
“Mfumo huu utawasaidia wateja wa MSD kupata taratibu za maombi ya dawa (order processing status) kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda, Vituo vya mauzo vya MSD,jambo ambalo litawaondolea usumbufu wa kusafiri kupata maelekezo, kwa kuwa mfumo huu unataarifa zote muhimu juu ya namna ya kupata mahitaji yao kutoka MSD” alisema.
Sianga aliongeza kuwa watejawa MSD wataweza kufahamu bei ya dawa (item price) mbalimbali zinazopatikana kwa wakati husika katika maghala ya MSD, kwani taarifa hizi ni muhimu kwao wakati wakupanga bajeti zao za manunuzi, na kufanya nakisi ya kiasi gani kitumike kununulia dawa husika.
Pamoja na hayo, alidokeza kuwa mfumo huo utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za miamala yao (customer statement) ili wafahamu kiasi cha pesa kilichopo kwenye akaunti zao MSD na kiasi cha fedha kilichotumika kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kwa wakati gani ambapo kupitia mfumo huo utakuwa unaondoa sintofahamu zilizokuwa zikijitokeza kipindi cha nyuma,kwa kuwa mfumo huu ni wa wazi na rahisi kutumia.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Afya ya kijiji cha Rwelu, Salum Chimbiaka alisema hivi sasa kila wanapokwenda kutibiwa dawa zimekuwa zikipatikana tofauti na zamani hivyo wanaishukuru serikali kwa kuwaondolea wananchi changamoto hiyo.
"Hivi sasa katika zahanati zetu wananchi wanaokwenda kutibiwa wamekuwa wengi kutokana na huduma nzuri wanayopata ukilinganisha na miaka ya nyumba ambapo walikuwa wakikimbilia kwenye zahanati za watu binafsi" alisema Chimbiaka.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mkoani humo maofisa hao wa MSD walitembelea Zahanati ya Rwelu, Naliendele na Kituo cha Afya Likombe.
No comments:
Post a Comment