Thursday, November 29, 2018

Matukio mbalimbali ya ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga (kushoto) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku nne. 
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup amekutana na Kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) katika ofisi za Wizara hiyo leo. Mazungumzo yao yalihusu kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan katika programu za kuboresha mifumo ya ukusanyaji fomu kodi Tanzania. 
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup katikati akiendelea na mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji hayupo pichani. kushoto ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Elisabeth Jacobsen 
Watumishi walioshiriki mazungumzo hayo, kushoto ni Bi. Tunsume Mwangolombe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zinajadiliwa katika mazungumzo hayo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga. 


Ziara katika Shirika la Reli Tanzania

Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup akiwa katika Shirika la Reli Tanzania. Mhe. Waziri alienda katika Shirika hilo kutembelea wahandisi wa kike wanaofadhiliwa na Serikali ya Norway. Katika programu hiyo Serikali ya Norway ishafadhili wahandisi wa kike 506 kwa gharama ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 4.2 kwa kipindi cha miaka 8. Ufadhili huo umepunguza uwiano wa wahindisi wa kiume na wakike kutoka 1:27 kabla ya programu kuanza na kufikia 1:10 kwa sasa. 
Wahandisi wa kike ambao wapo katika mafunzo ya vitendo wakitoa maelezo ya shughuli wanazofanya katika Shirika la Reli Tanzania. 
Ziara katika Viwanja vya Gymkhanas
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup akipiga mpira akiwa katika viwanja vya Gymkhanas. Mhe. Waziri alienda katika viwanja hivyo kujumuika na kuongea na watoto wa kike walioshindwa kumaliza masomo kwa sababu mbalimbali na kwa sasa Serikali ya Norway inatoa msaada wa fedha kwa ajili ya kuwafundisha watoto hao stadi za maisha. 
Baadhi ya watoto waliopo katika programu inayofadhiliwa na Norway ya kuwapatia stadi za maisha ijulikanayo Bonga Programu inayoendeshwa na Mfuko wa OCODE. 

No comments: