Tuesday, November 20, 2018

KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhifadhi ,kuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi wakati alipowatembelea jana katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa kwanza kushoto) akiwa ameongozana na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro akipewa maelezo wakati alipotembelea jana kabla ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipowatembelea jana. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakiamungalia Faru mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni faru mzee duniani

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Kanali Martin Kilugha mara baada ya kuwasili kati geti kuu la kuingia Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro . 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo na Juma Hamadi jinsi mfumo wa malipo unavyofanya kazi kwa watalii wanaoingia katika Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (PICHA NA LUSUNGU HELELA-WMU)

NA LUSUNGU HELELA .

Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu
 
Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi. 

Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi. 

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao. Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kanyasu ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ibuni vivutio vipya vya Utalii vitakavyosaidia kuongeza mapato kwa Serikali kwa kuzingatia majukumu makuu ya Taasisi. Kwa upande wake, Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro, Freddy Manongi amewahakikishia watumishi hao kuwa maslahi yao hayatabadilika na ikiwezekana yataongezwa kwa sababu uwajibikaji utaongezeka baada ya ujio wa Jeshi Usu Ameongeza kuwa mfumo wa Jeshi Usu haumaanishi kuwa Watumishi hawapaswi kupewa maslahi yao na badala yake yanahitaji kuboreshwa zaidi ili waweze kuwa na ari ya kufanya kazi katika kulinda Wanyamapori na Misitu nchini. 


” Kati ya masuala ambayo nayapigania yasiweze kubadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu ni maslahi yenu” amesema Dkt. Manongi. Jeshi USU lilizinduziwa rasmi tarehe 17 Novemba mwaka huu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Fort Ikoma wilayani Serengeti mkoa wa Mara.

No comments: