Makamu wa Rais wa Bunge la
Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati
alipotambulishwa Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia
ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini
Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la
Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha
ushirikiano baina ya pande zote mbili.
…………………..
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China
limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali ya
Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania
utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo
ya kuichumi
Hayo yamebainishwa na Makamu wa
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang
alipotembelea Darala la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam
lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na
China Major Bridge Engineering Company ujenzi ulioanza mwaka 2012 na
kukamilika April 2016.
Daraja hilo linalovuka mkondo wa
maji wa Kurasini hadi Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita
680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za
Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April
19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa
Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Ujenzi wa Daraja la Nyerere
ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari
uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na
kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye
sekta ya usafirishaji.Akizungumza katika ziara hiyo
Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang
amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za
kiuchumi kwa watu wa Tanzania.
“Nimefurahishwa na ujenzi wa
Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi
nzuri, kwa Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha
usafirishaji na kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara
hili” alisema Cai Defang Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu
wa China.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja
hilo kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia
Serikali mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa
zikienda kufanya shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.
“Tunashukuru Serikali kuendelea
kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa
asilimia mia moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani
fedha za makusanyo hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii
kupitia ujenzi wa miradi mingine” alisema William Erio wakati
akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China
alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.
No comments:
Post a Comment