Thursday, November 22, 2018

Jumia yakabidhi luninga, kutoa bodaboda Ijumaa hii!

Ni kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’
Luninga hiyo inauzwa shilingi 570,000 mtandaoni lakini mteja auziwa kwa shilingi 5,700!
Ijumaa hii bodaboda yenye thamani ya shilingi 1,850,000/- itauzwa kwa shilingi 18,500 tu kwa mteja atakayeipata. 

 Jumia imetangaza kutoa pikipiki aina ya Skymark yenye thamani ya shilingi 1,850,000 kupitia zoezi la ‘Treasure Hunt’ siku ya Ijumaa ya kesho. Zoezi hilo litafanyika kupitia App ya Jumia kwenye simu za mkononi pekee ili kutoa fursa kwa kila mtu kushiriki muda na mahali popote walipo. Mshindi mwenye bahati atakayefanikiwa kuipata pikipiki hiyo atauziwa kwa bei ya punguzo la asilimia 99 ambayo ni sawa ni shilingi 18,500 tu!

Jumia inaendesha kampeni yake kubwa kabisa ya mauzo ya mwaka inayokwenda kwa jina la Black Friday. Kampeni hii ilizinduliwa Novemba 16 na itafikia ukomo mnamo Desemba 7. Tofauti na miaka mingine ambayo Jumia hufanya Black Friday kwa siku moja tu ya Ijumaa ya Novemba 23, mwaka huu wateja watafaidi ofa za Black Friday kwa Ijumaa nne mfululizo. Lengo kubwa la kampeni hii ni kuwarahisishia wateja na watanzania kwa ujumla kufanya manunuzi yao hususani kipindi cha msimu wa sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya ambazo zipo njiani wiki chache zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey amefafanua kuwa, “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’, ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.”

“Hii ni fursa kwa watanzania kuanza na kujizoesha kutumia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandaoni. Kuna faida nyingi kufanya manunuzi mtandaoni kwa sababu unaokoa muda na gharama za kwenda dukani, unaweza kuperuzi bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji tofauti kwa wakati mmoja, muda wowote na mahali popote ulipo. Lakini kikubwa zaidi ni kwamba baada ya kufanya manunuzi utaletewa bidhaa zako mpaka hapo ulipo,” aliongezea Meneja Uhusiano wa Umma kutoka Jumia Tanzania.

“Leo tumekabidhi luninga ya kisasa kabisa ambapo mteja ameinunua kwa shilingi 5,700 badala ya bei ya shilingi 570,000 inayopatikana kwenye mtandao wetu. Tunatoa fursa nyingine kwa wale ambao hawakufanikiwa kushinda au kushiriki, kujishindia pikipiki aina ya Skymark ambayo itafichwa siku ya kesho ya Ijumaa ya Novemba 23 kuanzia saa 9 mchana,” alisema na kumalizia Bw. Geofrey, “Pikipiki hii ambayo inauzwa shilingi 1,850,000 kwenye mtandao wa Jumia itakabidhiwa kwa mteja atakayetakiwa kulipa shilingi 18,500 tu! Ili kuhakikisha kila mtanzania anashiriki zoezi hili, ‘Treasure Hunt’ itafanyika kupitia App yetu Jumia inayopatikana kwenye simu zote za mkononi, iwe ni Google Play au App Store. Ningependa kuwatakia kila la kheri katika zoezi la kesho, huwezi kujua namna zawadi hii itakavyobaidilisha maisha yako. Hakikisha unashiriki.”
Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Bw. Kijanga Geofrey akizungumza na Wanahabari leo jijini Dar kuhusu ufafanusi  wa  “zoezi la kuficha bidhaa mtandaoni ili wateja kuzisaka na kujishindia au ‘Treasure Hunt’,alisema na kuongeza kuwa ni mojawapo ya vitu vichache vinavyoendelea katika kampeni hii ya Black Friday. Kijanga amebainisha kuwa Miongoni mwa ofa zinazopatikana ni pamoja na punguzo la bei mpaka asilimia 70 na mauzo ya bidhaa maalum kwa bei nafuu zaidi ndani ya muda mfupi ndani ya siku au ‘Flash Sales.” 



No comments: