Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya Amana imetimiza miaka mitatu ya kufanya biashara na kutimiza ndoto ya watanzania kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo mbalimbali wakishirikiana na Kampuni ya Property International (PIL).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.
Rajab amesema kuwa, Katika mkopo huo watu wengi wameweza kunufaika kutumia viwanja hivyo kupata mkopo kupitia benki hiyo ili kuwezesha kuinua uchumi na kukuza biashara zao.
"Mteja anatakiwa atangulize asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kulipa kiasi kilichobaki kwa muda uziodi mwaka mmoja na nusu ila kwa sasa tumeongeza hadi miaka mitatu,"amesema Rajab.
Amesema, kutokana na kuwajali wateja wao wameongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kuwapunguzia faida toka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka mmoja.
Rajab ameeleza kuwa kuelekea Wiki ya huduma kwa wateja itakayoanza Novemba 19 mwaka huu, wateja watapata fursa ya kununua viwanja kwa punguzo maalum la bei na kutakuwa na mwakilishi kutoka PIL ndani ya wiki nzima ya huduma kwa wateja katika matawi yote Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Property International (PIL), George Obad0 amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya Amana na kufanikisha watanzania wengi kupata viwanja vilivyopimwa pia wamekuwa wanafanya marekebisho ya barabara kwa kiwango cha Changarawe ili kufika kwenye maeneo yaliyo na viwanja.
Obad0 amesema, mbali na hilo kwa sasa viwanja vipo katika miradi ya Kimbiji Sea View Kigamboni, Magodani Mkuranga, Mapinduzi Residence, Chekeni Farm Mwasonga -Tundwi, Fukayose Residence Barabara ya Bagamoyo -Msata, The Dar es Salaam Automobile Zone (DAZ), Riverside Residence, Coco Palm, Royal Palm Mwasonga, African Palm Estate na Dege Residence.
Mmoja wa wateja walionufaika na ukopeshaji wa viwanja hivyo na kukabidhiwa hati yake leo, Aisha Sufana amesema kuwa ameweza kumilili kiwanja ambacho hakutegemea kukipata tena kikiwa cha thamani kubwa kulingana na kipato chake ambapo yeye ni mjasiriamali wa kawaida.
Aisha amesema kuwa amekabidhiwa hati yake na kwa sasa anaweza kuitumia kama dhamana ya kuchukulia mkopo na kuendeleza biashara zake.
Amana Bank wamekabidhi hati kwa wateja watatu waliofanikiwa kumaliza mkopo wao wa viwanja .
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab akizungumza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano wa Benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa mkuu Mwendeshaji wa Propert International Ltd(PIL) George Obado akizunguza na wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya Amana kuhusu utoaji wa mikopo ya viwanja kwa wateja wa benki hiyo leo wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano wao.
Mmoja wa wateja wa benki ya Amana Stephano Matesi akipokea hati ya kiwanja kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab leo kwenye maadhimisho ya miaka mitatu ya ushirikiano kati ya benki hiyo na kampuni ya Propert International Ltd(PIL)
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab(kushoto) akikata keki ya maadhimisho ya miaka mitatu kati ya benki hiyo na kampuni ya Property International Ltd(PIL) pamoja na Afisa mkuu Mwendeshaji wa Propert International Ltd(PIL) George Obado na Baadhi ya wateja wa Viwanja
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment