Saturday, October 20, 2018

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 25 KWA WATUMISHI CHAMWINO



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya wilaya Chamwino kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma majina ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambao hawaishi kwenye Kituo chao cha kazi cha Chamwino badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chamwino, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga ordha ya watumishi ambao hawaishi kwenye kituo chao cha kazi cha Chamwino na badala yake wanaishi jijini Dodoma. Alikuwa katika mazungumzo na watumishi wa Halmashauri hiyo kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino wakimshangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kuzungumza na watumishi hao, Oktoba 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




*Ni wale washio nje ya kituo, wawe wamehamia ifikapo Desemba 15


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaametoa siku 25 kwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

Pia amemkabidhi Mkuu wa wilaya hiyo Bibi Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino ambao wanaishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Oktoba 20, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Chamwino.

“Ifikapo Desemba 15 mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi.” Waziri Mkuu amesema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa kwenye utumishi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato. Amesema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielekroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

Pia Waziri Mkuu amekagua barabara za mitaa katika mji wa Chamwino zenye urefu wa kilomita 3.5 zinazojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo. Baada ya kukagua barabara hizo, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa miundombinu ya majengo ya kituo cha Chamwino na kisha kuzungumza na wananchi waliofika kituoni hapo.

No comments: