Sunday, October 21, 2018

WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Na Frankius Cleophace, Serengeti.

Wasichana zaidi ya  400 (Mianne) wa shule za sekondari wilayani Serengeti Mkoani Mara wamepatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike pamoja na elimu ya Afya ya Uzazi na utunzaji wa Mazingira kwa lengo la kukomboa Mwanamke huku wengine 1160 wakitarajia kupatiwa elimu hiyo. Hayo yamebainishwa na Frida Mollel ambaye ni  Meneja Idara ya Maendekeo ya jamii kampuni ya  Singita Grumeti Fund iliyopo wilayani  Serengeti  Mkoani Mara  katika viwanja shule ya Msingi Makundusi baada ya kutoka Shule ya Msingi Natta kwa kukikbia mbio fupi.

Frida amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na wanakijiji kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Ikorongo Grumeti Reserves ili kuendelea kutunza mazingira na jamii kuondokana na ujangiri ili kulinda hifadhi pamoja na wanyama ili kunufaisha kizazi kijacho.
Meneja Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji na mila kandamizi kwa wasichana pamoja na wanawake katika viwanja vya shule ya Msingi Natta wilayani Serengeti mkoani Mara.

Licha ya kutolewa kwa elimu ya kutunza mazingira Frida amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa elimu ya kupinga suala zima la ukeketaji na mila kandamizi ambazo zinazidi kundamiza mwanamke pamoja  na msichana mpaka kushindwa kutimiza ndo zake ambapo elimu hiyo imeanza kutolewa tangu mwaka jana lengo ni kukomboa mwanamke.

“Mwaka jana tuliweza kukutana na wasichana wakatupa changamoto zinazowakumba kipindi cha ukeketaji na mwaka huu Serengeti kulingana na mila na desturi watakeketa sasa tumeona tutumie fursa hii kutoa elimu ili kukomboa mtoto wa kike ukiangalia pia kuna wanawake ambao wametoka nje ya nchi ya Tanzania kwa maana ya Afirika kusini na Marekani ili kutuunga mkono lengo ni kutoa hamasa kubwa kwa mabinti hao pia wameweza kukimbia mbio fupi ni wasichana hao alisema Frida.” alisema Frida.
Rnonda Vetere Kutoka New York City Marekani akiongea na wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu mwanamke kijiamini ambapo amewasihi kudhubutu na kujiamini kwa lengo la kufanikiwa huku wakiendelea kutoa elimu juu ya kupinga mila kandamizi.

Katika kutoa elimu hiyo na kutoa hamasa kwa mabinti hao baadhi ya washiriki ambao wamekuwa wakitoa elimu wametoka nje ya Nchi huku baadhi yao wakitoka  Afrika Kusini, na Marekani  Rnonda Vetere kutoka New york City Nchini  Marekani  amezidi kuhamasisha wanawake Nchini Tanzaniakuendelea  kujiamini na kudhubutu kwa lengo la kupata mafanikio ili kuendeleza mapinduzi katika kutokomeza Mila kandamizao ukiwemo Ukeketaji kwa mtoto wa kike.

Pia katika kuongeza hamasa wanafunzi hao zaidi ya Mianne wamefanya mazoezi ya kikimbia mbio fupi kwa kushirikiana na wageni hao huku wakitembelea vimbanda mbalimbali na kupatiwa elimu tofauti kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waendelee kuwa mabalozi wazuri wakutoa elinu hiyo vijijini na mashuleni.
Mmoja wa wanafunzi kutoka Sekondari akikabidhiwa zawadi kwa kufanya vizuri katika Masomo yake.

Bahati  Sostenes ambaye ni Afisa elimu katika kampuni ya Singita Grumeti Fund  amesema kuwa wameendelea kusaidia watoto wa kike taulo za kike ili waendelee na masomo huku Mwalimu Monica  Paschal kutoka Shule ya sekondari Makundusi akieleza changamoto zinazowakumba watoto wa kike pale wanapokeketwa wakiwa shuleni kuwa suala la utoro ni changamoto kubwa msimu wa ukeketaji.

Aidha Frida ameongeza kuwa kama kampuni ya Singita Grumeti Fund wamekuwa wakisaidia ufadhili wa  masomo kwa wanafunzi mbalimbali  hususani wa kike ili kukomboa Mwanamke ambapo pia  wanafunzi ambao wameshiriki  wametoa shukrani juu ya elimu hiyo wanayoipata kupitia kampuni hiyo  huku wakitupia lawana wazazi na walezi kuendelea kuwakeketaja na kusababisha kuzima ndoto zao.
Mmoja wa wanafunzi akikimbia na Mgeni kutoka Nje ya Nchi ambao wameshiriki pia kutoa elimu juu ya Afya ya Uzazi, Mazingira.
Bahati Sostenes ambaye ni Afisa elimu katika kampuni ya Singita Grumeti Fund akitoa elimu ya utunzaji wa mazingira baada ya wanafunzi hao kutembelea kibanda hicho.
Wanafunzi wanaendelea kupatiwa elimu mbalimbali ya kupinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike wilayani Serengeti mkoani Mara ili kuondoa mimba za utotoni na ndoa za utotoni zinazosababishwa na ukeketaji.
Picha ya pamoja kati ya wageni waliotoka nje ya nchi ya Tanzania ikiwemo Marekani na Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliopatiwa zawadi kwa kufanya vizuri katika masomo yao.

No comments: