Sunday, October 21, 2018

ZIARA YA DKT NDUGULILE KATIKA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MVOMERO MOROGORO

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongozana na Wananchi wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero kukagua mradi wa skimu ya umwagiliaji uanondeshwa na Serikali ya kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea taarifa ya mradi wa skimu ya umwagiliaji uanondeshwa na serikali ya kijiji cha Wami Luwindo Dakawa Wilayani Mvomero kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Bw. Frolence Laurent Kyombo.
Wajasiliamali wadogo kutoka vikundi vya mbalimbali vilivyopo wilayani Mvomero wakitoa maelezo kuhusu bidhaa wanazozalisha kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Wilaya hiyo jana kujionea kazi za vikundi hivyo wakati wa ziara yake ya siku tatu Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi milioni moja kwa Mwenyekiti Skimu ya Umwagiliaji wa kijiji cha Wami Luwindo kilichopo Dakawa Wilaya ya Mvomero Bw. Juma Achumu kama mchango wa Wizara yake kuwezesha na kuamsha hari ya Wananchi kijiletea maendeleo.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………….

Na Mwandishi wetu Morogoro

Seriklai imeziagiza Mamlaka ya Udhiti Ubora Tanzania (TBS), Mamlaka ya Udhiti wa ubora wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na SIDO kuwapa elimu Wanawake wajasiliamali wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ili kuongezea thamani katika bidhaa zao kwa kuwapa wabunifu na kuhakikisha bidhaa zao zinakuwa vifungashio vyenye ubora ili ziweze kushindana katika soko na bidhaa nyingine.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipotembelea vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Wilaya ya Mvomero katika ziara yake Mkoani Morogoro kuangalia utoaji huduma za Afya na Maendeleo ya Jamii.

Pamoja na mambo mengine Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Ndugulile amesema ili wanawake hao waweze kufikia malengo yao na kukuza biashara yao lazima bidhaa ziwe na nembo ya biashara ambayo itatambulisha bidhaa zao na kusaidia kuvutia wateja.

‘’Wekeni nembo katika bidhaa zenu na serikali ya Wilaya iwasaidie ili muweze kuwa na viwanda vidogo vya uzalishaji mali jambo ambalo lipo pia katika Nchi zinazoendelea ambapo viwanda vidogo vimekuwa vikisaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi mfano mkiongezea thamani bidhaa zenu na kuzipa nembo ya Movomero itakuwa bora zaidi’’. Alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Naibu waziri huyo amewataka viongozi wa Wilaya Mvomero kutafuta namna ya kuwapa elimu ya kutengeneza vifungashio wajasiliamali wadogo hao ilikuweza kufikia hadhima ya serikali ya viwanda.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero Bw. Florence Kyombo akitoa taarifa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na uhamasishaji wa wanawake kujiunga na vikundi vya kiuchumi Wilayani Mvumero alisema utoaji wa mikopo kwa wanawake utawezesha wananchi kuajiliwa, kuajili na kuongeza pato la familia.

Bw. Kyombo katika taarifa yake hiyo kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile alisema Wilaya yake kwa mwaka 2017/18 ilitoa mikopo kwa wanawake kiasi cha Tsh.84 kwa vikundi vya wanawake 44 vyenye wanaufaika 757 na vijana pia kiasi Tsh.57.4 milioni kwa vikundi vya vijana 15 vyenye wanufaika 184.

Akizungumzia kuhusu kikundi mlezi Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mboni Mgaza amesema kuwa dhana ya hiyo imeanzishwa na Wizara kwa lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali waliofanikiwa kuwasaidia wale ambao wanaanza ili kuinua katika biashara na ili wanawake kuweza kuinuka kiuchumi.

No comments: