Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii
NAIBU
Waziri wa kilimo na uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega
amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya
maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu
yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland
na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa
za uwekezaji katika sekta mbalimbali.
Aidha
ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya
chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika
suala la ufugaji wa kuku.Pia amewataka kushirikiana na
kufanya kazi kwa pamoja na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi
wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa
ushirikiano wao kupitia vyama vyao.
Ulega
amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi
sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa
ili kuweza kuendeleza shughuli za hizo.Kuhusiana na
changamoto zilizotolewa na wafugaji hao hasa katika mashudu na soya
ambazo huagizwa kutoka nje Ulega amesema kuwa maandalizi yameanza katika
nyanda za juu kusini ambako soya zimelimwa na wanavutia uwekezaji
katika usindikaji ili kuweza kuvutia uwekezaji wa kuchakata soya na
kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.
Kuhusiana
na machinjio zinazochinja kuku Ulega amesema kuwa sehemu hizo zimekuwa
na ubora wa chini sana na amewataka wahakikishe wanaboresha machinjio
hayo yanayosimamiwa na halmashauri na manispaa hasa kwa kuzingatia
wanaweka sehemu ya machinjio ya kuku ili kuleta thamani.
Mwenyekiti
wa chama cha ndege wafugwao Harko Bhaghat amemshukuru Naibu waziri na
wizara kwa ujumla kwa kutoa kipaumbele kwa wafugaji na kusema kuwa hadi
sasa wamepata mafanikio makubwa na kubwa zaidi ni baada ya serikali
kuondoa tozo katika bidhaa za mifugo.
Bhaghati amewataka wafugaji kujisajili ili waweze kupata fursa mbalimbali za kuendeleza soko la ndege wafugwao hasa kuku.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa
ndege wafugwao, katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya ndege wafugwao
nchini jana jijini Dar es Salaam . (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu
ya Jamii)
Mwenyekiti
wa chama cha wafugaji wa ndege Harko Bhaghati akisoma risala mbele ya
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega.
Mtaalamu
na mshauri wa mifugo kutoka kampuni ya Animal Care Dkt. Bakari Mwanga
akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega
kuhusu uzalishaji na utunzaji wa mifugo unaofanywa na kampuni yao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Sehemu ya wafugaji waliojitokeza ili kupata semina na mafunzo kuhusiana na ufugaji wa kuku.
No comments:
Post a Comment