Friday, October 26, 2018

Ufungaji wa flow meters katika bandari zote nchini kukamilika hivi karibuni.Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters. kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wa wizara na taasisi zilizochini yake wakiwa katika wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kilichofanyika jijini Dodoma na iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uwagizaji Mafuta kwa Pamoja( PBPA), Mhandisi Erasto Simon (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula,( katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Nishati, wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.


Na Zuena Msuya, Dodoma

Serikali imesema kuwa taratibu za ufungaji wa flow meter katika bandari zote nchini ziko katika hatua za mwisho baada ya taratibu zote kukamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula, ambaye alihoji mambo kadhaa kubwa likiwa ni hatua gani zimefikiwa katika zoezi za ufungaji flow Meter katika bandari kuu nchini ili kudhibiti upotevu wa mafuta na kuongeza mapato ya serikali.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alieleza kuwa tayari hatua mbalimbali zimekwisha kuchukuliwa ili kukamilisha zoezi hilo, baada ya Mawaziri wa wizara tano, zinazoshirikiana katika sekta hiyo kukutana pamoja na kuweka ratatibu za kuimarisha na kudhibiti upotevu wa mafuta na mapato ya serikali.

Dkt. Kalemani alieleza wazi kuwa, kwa sasa Flow Meters zipo kwenye mchakato wa Manunuzi, ambapo zoezi hilo linakwenda haraka na muda si mrefu litakamika na kulitolea taarifa.“ Zoezi la kununua Flow Meter linaendelea vizuri na kwa kasi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ndiyo ilipewa jukumu la kusimamia zoezi hilo, kwa kuwa sekta hii inahusisha Wizara tano, ikiwemo Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Wizara ya Nishati yenyewe:, ufungaji wa flow meter hizo utafanyika katika bandari zote nchini ikiwemo Dar es salaam, Tanga pamoja na Mtwara”, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Kuhusu suala la upokeaji wa mafuta kwa pamoja, Dkt. Kalemani alisema , kupitia Wakala wa Serikali wa Uwagizaji Mafuta kwa Pamoja( PBPA) na Kampuni zinazofanya biashara ya mafuta nchini( OMCs) unaendelea kukamilisha taratibu za kuanzisha mfumo wa upokeaji wa mafuta sehemu moja unaofahamika kama Single Receiving Terminal (SRT).

Alisema kuwepo kwa utaratibu huo kutapunguza muda wa meli kusubiri kushusha mafuta hivyo kupunguza upotevu wa mafuta. Pia PBPA kwa kushirikiana na Taasisi za serikali ikiwemo Mamlaka ya Bandari Tanzania( TPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji( EWURA) pamoja na OMCs unaendelea kuimarisha mfumo wa kitaalam ili mabomba yote yaunganishwe kwenye mfumo ulio rahisi kuuendesha kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.

Akizungumzia wa kampuni ya kuhifadhi mafuta ya TIPPA, pamoja na Shirika la Maendeleo la Petroli Nchini( TPBD)Dkt. Kalemani alisema kuwa kinachofanyika sasa ni kuangalia uwezekano wa kupanua miundombinu ya kulingana na uhitaji wa mafuta .

Aidha aliwaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa, wameweka mfumo wa kieletroniki ili kulinda mindombinu ya mabomba yanayotoka baharini kuelekea kwenye maghala ya kupokelea mafuta ili yasitobolewe.Mfumo huo wa kieletroniki utakuwa ukitoa taarifa iwapo msukumo wa mafuta utapungua wakati wote wa zoezi la kupakuaji wa mafuta.

No comments: