Friday, October 26, 2018

TANAPA NA WADAU WA UTALII WAFANYA KAMPENI YA KUTANGAZA VIVUTIO KATIKA JIJI LA MWANZA

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii. WADAU wa Utalii kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika jiji la Mwanza leo wameanza kampeni ya siku tatu ijulikanayo kama “Discover the Treasures of Mwanza” itakayoshirikisha zaidi ya wanafunzi 800 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu. 
Lengo la kampeni hii inayotarajia kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane linatajwa kuwa ni kutoa fursa kwa wanafunzi hao wa elimu ya juu kutambua umuhimu wa kutembelea rasilimali zilizopo nchini na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utalii wa ndani. 
 Akizungumzia tukio hili mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(SAUT),Judith Wanda,anasema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza leo oktoba 26 hadi 28 mwaka huu. 
 Wanda amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa kwanza watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala ya uhifadhi na utalii wa ndani pamoja na namna bora ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini. 
 "Vyuo vinaanza udahili hivyo tumelenga wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya juu na tunatarajia kutumia fursa hiyo kuwafundisha wanafunzi kutembelea vivutio na rasilimali zilizopo nchini kama njia ya kujifunza na tunaamini hawa wataenda kuelimisha jamii umuhimu wa uhifadhi na utalii wa ndani.
 "Kampeni hii ya siku tatu imelenga kukutanisha wanafunzi 800 na kila mwanafunzi atajigharamia kiasi cha Sh 8,800 kwa ajili ya usafiri na shughuli nyingine hifadhini(Saanane),tulishawahi kufanya kampeni ya kwanza na tulikuwa tukihusisha wanafunzi wa maeneo ya Mwanza," 
 Awali Mkuu wa Idara ya Utalii katika hifadhi hiyo ya Saanane,Ikwabi Koroso,anasema hali ya utalii hifadhini humo imeimarika ambapo tangu ilipotangazwa Julai mwaka 2013 kuwa hifadhi ilikuwa na wastani wa wageni 4,000 kwa mwaka ila kwa sasa ni wastani wa wageni 15,000 kwa mwaka. 
 "Hali ya utalii imezidi kuimarika,kati ya wageni hao asilimia 96 ni wale wanaotoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na mapato yanazidi kukua kulingana na idadi ya wageni hivyo tunatumai kupitia kampeni hii itaongeza idadi ya watalii katika hifadhi yetu ambayo ni ndogo kuliko hifadhi zote,"anasema 
 Kuhusu usalama kwa watalii,Mkuu huyo anawahakikishia watalii kuwa usafiri huo wa kwenye maji uko salama na kuwa wanachukua tahadhari kubwa ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa vyombo vya usafiri. "Tunashirikiana na wadau wengine kutangaza utalii na tunaamini kupitia kampeni hii tutaongeza idadi kubwa ya watalii katika hifadhi yetu na maeneo mengine yenye vivutio katika ukanda huu," 
 Naye Mkuu wa TTB Kanda ya Ziwa,Gloria Mnihambo,anasema awali kabla ya kuanzishwa kwa ofisi katika Kanda hiyo idadi ndogo ya watalii wa ndani walikuwa wakitembelea Hifadhi na vivutio mbalimbali. 
 Anasema kuwa hivi sasa mwamko umekuwa mkubwa kwa watalii ndani kutembelea vivutio hivyo baada ya kushirikiana na wadau wengine na kuwa kupitia kampeni hiyo wataendelea kutangaza vivutio mbalimbaliili kuongeza idadi hiyo. 

Kundi la Waandishi wa Habari wakiwa katika boti maalumu kwa ajili ya safari ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Muonekano wa Mawe yaliyobebana ni miongoni mwa vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Sannane.
Muinekano wa lango la kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Baadhi ya Watalii wa ndani wakiwa katika Lango la kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiw acha Saanane kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi hiyo.  
Baadhi ya Wageni wakipumzika katika moja ya maeneo yaliyopo katika Hifadhi hiyo.
Baadhi ya Vivutio vilivyomo ndani ya Hifadhi hiyo ,akiwemo ndege aina ya Tausi na Mnyama Simba.
Katika Hifadhi hiyo lipo ene maalum kwaa ajili ya kuweka kambi wakati wa kfanya shughuli ya utalii katika Hifadhi hiyo.
Eneo hili linajulikana kama Kona ya Siri "Scret Corner " iliyipo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saaanane ambayo imekuwa ikitumiwa na wanandoa kwa ajili ya kuombana msamaha.
Eneo hili linajulikana kama Jiwe la Kugusa "Touch Stone" ni moja la eneo ambalo watalii wa ndani wamekuwa wakitumia kupata Taswira .
Mti wenye muonekano wa mnyama Twiga "Giraffe Tree" ni kivutio kingine ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kilichopo jijini Mwanza.
Eneo hili limo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ambalo linajulikana kama jiwe la kuruka "Jump Stone" limekuwa ni kuvutio kwa wageni walitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kuchukua Taswira wakati wakiruka.
Mmoja waMhadhiri wa Chuo Kikuu cha St ,Agustine kilichopo jijini Mwanza,Judith Wanda akizungumza na wanahabri kuhusu kampeni inayozinduliwa leo ya kutangaza Vivutio vya Utalii katika jiji la Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ,Ikwabi Koroso akizungumza kuhusu kuanza kwa kampeni hiyo.

No comments: