Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar akitoa hotuba wakati wa hafla ya uzunduzi wa miundo mbinu ya vyoo katika shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia mjema, Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu, walimu, wanafunzi, Maofisa ma maofisa kutoka taasisi ya HMT
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema( katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Vyoo bora 12 na vyumba Viwili kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaa, Wengine kwenye picha ni mwenyekiti wa Hassan Maajar Trust (TMT) Balozi Mwanaidi Sinare Maajar (wapili kulia) Mkuu wa shule ya msingi Pugu Kajiungeni,Ropiana Alponce (Kushoto) pamoja na viongozi wengine, Msaada huo umejengwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia wageni waalika katika hafla hiyo.
Wanafunzi wasichana wakipokea baadhi ya zawadi zilizotolewa na marafiki wa taasisi ya HMT wakati wa hafla hiyo.
Mgeni rasmi akikagua miundombinu ya choo cha kisasa kilichojengwa na HMT chini ya mpango wake wa Vyoo Bora kwa Kila shule
Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT), imeendeleza dhamira yake ya kuboresha mazingira ya shule za msingi nchini, ambapo imekabidhi jengo la vyoo shule ya msingi Pugu Kajiungeni, wilaya ya Ilala, Dar es Salaam. Jengo hilo lililogharimu jumla ya Shillingi milioni 65,000.00 lina vyumba 12 na sehemu maalumu kwa wavulana -urinals, ambapo vyumba 2 ni kwa ajili ya ya watoto wenye ulemavu na chumba cha staha kimoja (Dignity Room) kwa ajili ya wasichana wenye mahitaji ya staha.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Maajar, alikabidhi vyoo
hivyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi. Rophina Aloyce Kawishe, katika
hafla fupi iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema,
ambaye alikuwa mgeni rasmi, walimu, wanafunzi, na wawakilishi kutoka
Shirika la Water Aid.
Akiongea
katika hafla hiyo, Balozi Maajar amesema “Hii ni mara ya kwanza kwa HMT
kujenga vyoo vya shule, na tumefurahia kukamilisha mradi huu wa kwanza.
Kwa kipindi kirefu nyuma, HMT ilikuwa inajulikana kwa kampeni yake
kubwa ya ‘Dawati Kwa Kila Mtoto’ ambayo imefanikiwa kwa kutoa madawati
10,000, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 30,000 katika mikoa 13 nchini.
Tuliona
vilevile vile kuna changamoto ya uhaba wa vyoo mashuleni. Imekuwa fursa
nyingine ya Taasisi ya HMT na wafadhili wake kuunga nguvu kwa pamoja
kwa kampeni mpya yenye kauli mbiu, Vyoo Bora Kila Shule. Aidha amesema,
kila safari ni hatua ya kwanza na kwa mradi huu ndiyo hatua ya kwanza
kwa HMT kutimiza lengo la kujenga vyoo shule za msingi zilizo na
mahitaji na hasa shule zilizo na idadi kubwa ya wanafunzi wenye
ulemavu.
Alisema
Kupitia hafla tofauti za ukusanyaji fedha kama vile ‘Fundraising Gala’
na ‘Matembezi ya Hiyari’, HMT kupitia kampeni ya Dawati kwa kila Mtoto
ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha umma kuona kuwa wajibu wa
kuboresha mazingira ya shule zetu si wa serikali pekee na kuweza
kuchangia madawati hadi pale serikali ilipolivalia njuga tatizo lile.
Kwa HMT ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya watoto wetu siku hizi
wakiwa hawakai tena chini.
Kwa
kampeni mpya, Vyoo Bora Kila Shule HMT inakusudia kuwasha tena mshumaa
kuangazia tatizo la vyoo kwa kuhamasisha umma kuchangia ujenzi wa vyoo
katika shule za msingi zilizo na wanafunzi wengi na vyoo vichache. Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema, aliipongeza, HMT, kwa kuamua
kuzikabili changamoto za kuboresha mazingira ya elimu kwa kutoa misaada
ya madawati, huduma za maktaba na kujenga miundombinu ya vyoo.
“Kwa
niaba ya serikali nawapongeza kwa jitihada mnazofanya kuboresha
mazingira ya kupata elimu mashuleni” alisema. Taasis ya WaterAid
wameisaidia shule kwa kuipa vifaa vya kuvunia maji ya mvua, jambo ambalo
limeongeza ubora wa vyoo vilivyojengwa na HMT kwa sababu mazingira ya
vyoo yatakuwa masafi naya afya zaidi.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya msingi ya Pugu Kajiungeni, Bi. Rophina Aloyce Kawishe,
ameishukuru taasisi ya HMT kwa kutoa msaada huo ambao alisema
utawezesha wanafunzi wa shule hiyo kusomea katika mazingira rafiki
kutokana na kuwa na miundombinu bora ya vyoo na madarasa “Ukosefu wa
vyoo vya kutosha kwa muda mrefu imekuwa ni changamoto kubwa katika shule
zetu, tunawashukru kwa msaada huu”, alisema.
Taasisi
ya Hassan Maajar inafanya maandalizi ya kujenga majengo mengine mawili
ya vyoo shule za msingi Nia Njema na Majengo zilizoko Bagamoyo, mkoa wa
Pwani. Ujenzi unatarajiwa kuanza mwezi huu wa kumi na HMT imetenga kiasi
cha Shillingi 140 Milioni kwa ajili ya ujenzi huo.
Taasisi
ya HMT inajulikana zaidi kwa kampeni yake ya Dawati kwa Kila Mtoto
ikiwa ni makakti wa kutimiza ndoto yake ya kuboresha mazingira ya
kusomea katika shule za msingi nchini. Tangu kuanzishwa kwake, imekuwa
ikihamasisha umma na kuchangia madawati, kuboresha maktaba na kutoa
vitabu, na hasa kwa watoto wa madarasa ya awali ili kujenga tabia ya
kujisomea, vile vile kuongeza ufahamu juu ya changamoto zinazowakabili
wanafunzi wakiwa shuleni.
HMT
inajivunia mafanikio kwa kuona hamasa kwa watu binafsi, mashirika ya
umma na hadi serikali kuamua kulivalia njuga tatizo al upungufu wa
madawati shuleni. Kwa kampeni hii mpya Vyoo Bora Kila Shule, HMT ina
imani watu wengi wataendelea kuhamasika kushiriki kwa kutambua kuwa ni
jukukumu letu sote kuondoa tatizo la vyoo mashuleni na siyo tu kazi ya
serikali peke yake.
No comments:
Post a Comment