Leo
26/10/2018 Majira ya Saa tatu na nusu asubuhi tumepata changamoto ya
kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani
katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru ambapo
katika tukio hilo tumeweza Kuokoa Mwanafunzi Mmoja wa Kiume aliepata
majeraha sehemu na bado tunaendelea na jitahada za kuondoa kifusi
kilichochanganyikana na matofali ambacho kimezama katika Shimo la choo
kilichokuwa na matundu 20
Katika kukabiliana na Changamoto
Iliyotokea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiambatana na
Katibu Katibu tawala wa Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Arusha
walifika kwenye eneo la tukio na kuanza kazi ya kuratibu jitihada za
uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na Zimamoto pamoja na mamia
ya wananchi wa kata ya kimnyaki ambapo walifanikiwa kumuokoa mwananfunzi
Mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani
kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na
jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo
hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa
na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
Katika Eneo la tukio
kwanza tulilazimika kurejesha hali ya Amani na kutuliza taharuki za
wananchi ambao baadhi Wana watoto wanaosoma katika shule hiyo na kutoa
nafasi kwa vikosi vya ukoaji kuendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi
wengine Kutokana na kutokupatikana kwa Taarifa za awali zinazoonyesha
idadi ya Wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.
Kutokana
na shule hiyo kuwa na choo kimoja chenye matundu ishirini ambacho
ndicho kilikuwa pekee kwa shule hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya
Arumeru kuchukua hatua za kuzungumza na Uongozi wa Kanisa la KKKT
usharika wa seliani na kuomba shule kutumia vyoo vya Kanisani ombi
ambalo lilikubaliwa na *Mkuu wa jimbo la Arusha Magharibi Mchungaji
Philemon Joseph Mollel ambae aliungana na Mkuu wa Wilaya katika zoezi a
uokoaji na hivyo kuondoa Mashaka ya kufungwa kwa shule.
Kutokana
na kadhia hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro
kuzungumza na wananchi waliojitokeza ambapo katika mazungumzo yake
aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la
utoaji wa kifusi ili kujirisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.
Awali
kwa upande wao baadhi ya wananchi waliungana na Mkuu wa Wilaya katika
kuchanga Fedha kwa ajili ya kuanza Mikakati ya Ujenzi wa choo kingine
ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa
Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa
wingi na wananchi waliotoa Fedha zao.
Awali Mhe Muro alilazimika
kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika hospitali ya seliani na
kumjulia hali uku akiongozana na viongozi mbalimbali.
Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
26/10/2018
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akimjulia hali mmoja wa wanafunzi aliyejuruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi kufuatia kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhutia tukio hilo,ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujiridhisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao kufuatia tukio la kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru
No comments:
Post a Comment