Wednesday, October 24, 2018

NDITIYE AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA TEHEMA, KAMPUNI YA BCX YAWA KIVUTIO KWA WADAU

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye  amezindua mkutano wa siku 3 wa wanatehama ili  kujadili masuala ya tehama na maendeleo ya viwanda nchini.

Nditiye amesema kuwa mkutano huo utawasaidia wananchi kutapata uelewa wa matumizi bora na usalama katika mitandao ya kijamii na amewataka wanatehama wote kutambulika na vyombo husika na wao kama serikali wanafanya kazi na watakaovuruga tasnia hiyo hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Kwa upande wao kampuni ya Bussiness Connexion (BCX)  wanaojihusisha na masuala ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa mbalimbali pamoja na komputa za aina zote  kutoka makampuni ya HP  na DELL, kutoa wataalamu wa kompyuta kwa makampuni, kutengeneza programu za simu na huduma za malipo wameshiriki semina hizo na kuwa kivutio kwa wadau wengi wa tehama.

Akizungumza na blogu ya jamii Afisa mauzo na masoko wa BCX  Justine Lawena amesema kuwa wameshiriki semina hiyo katika kujitangaza na kuonesha uwezo wao kwa serikali na wadau wa tehama na wao kama kampuni wana wataalamu wa kompyuta wakutosha  hivyo serikali na taasisi binafsi kutumia fursa hiyo.

Ameeleza kuwa katika kuendeleza sekta ya tehama wanatoa huduma za kuuza na kutengeneza mashine za kutoa pesa (ATM) na hadi sasa wanamiliki na kuendesha mashine zaidi ya 200 nchini.

Aidha amesema kuwa katika kurahisha huduma za malipo kwa kipindi cha mwaka mmoja wamekuwa wakifanya majaribio kupitia kadi zao za uhuru pay ambazo huwasaidia wananchi  kulipa nauli katika usafiri wa daladala na majaribio yalifanywa kwenye daladala zinazofanya safari kutoka Kivukoni hadi Tegeta nyuki na imeonesha mafanikio makubwa na wamejipanga kueneza huduma hiyo katika maeneo mbalimbali.

Akizungumzia mafanikio ya kampuni yao Lawena amesema kuwa hadi sasa wanatoa huduma za kibenki kwa benki 28 kupitia huduma ya umoja switch na kutoa huduma za kibenki kupitia mawakala na kubwa zaidi ni kumiliki na kuendesha zaidi ya mashine za ATM zaidi 200 nchini.

Lawena amewashauri na kuwahimiza wamiliki wa mabenki nchini kutumia huduma zao kwani wanauwezo wa kufungua matawi kupitia (ATM) katika maeneo yote nchini na kuziendesha ipasavyo.
 Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya BCX  Justine Lawena akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye  katika banda lao katika maonesho ya wadau wa tehama nchini.
 Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya BCX Justine Lawena (kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau waliotembelea banda lao.


Afisa mauzo na masoko wa kampuni ya Bussiness connexion (BCX) Justine Lawena (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian0-Uchukuzi na Mawasiliamo Atashasta Nditiye wakati wa ufunguzi wa semina ya tehama kwa wadau.

No comments: