Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
KATIKA jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni International Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio hizo ambaye pia ni kocha wa michezo ya riadha na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu Tanzania alisema, Lengo kuu la “Kigamboni International Marathon” ni kuchochea shughuri za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji,Biashara na vivutio vya kitalii Vilivyopo Kigamboni na maeneo ya karibu, Kuimarisha Afya pia Kuhamasisha michezo ya Riadha kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.
Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa „kigamboni International Marathon‟ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.
Ni ukweli ulio wazi ya kuwa Kigamboni imezunguukwa na maeneo mazuri zaidi ya kimichezo, Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote ile Jijini Dar es saalam na hiyo ni sababu moja wapo inayotupelekea kuamini kuwa „Kigamboni International Marathon‟ ni miongoni mwa mbio bora Tanzania yenye lengo la wakimbiaji wazuri watakao watakaoleta ushindani mkubwa katika Mchezo huu wa riadha Duniani kote.
Kigamboni International Marathon itafanyika tarehe 2 mwezi wa 12, 2018 Katika sehemu yenye mandhari nzuri nay a kipekee kabisa Afrika Mashariki ‘Fun City – Theme and Water Park’ ili kutoa nafasi kwa washiriki kuburudika na michezo mbali mbali ikiwemo kuogelea baada ya mbio. ikiwa na Mbio za urefu wa kilomita 21(Half Marathon), Kilomita 10 na Mbio kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na mazoezi ya mara kwa mara (Fun Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo Medali za dhahabu, Silver na Gold pia Pesa Taslimu kwa washindi.
Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya „kigamboni International Marathon‟ natanguliza Shukrani kwa wadau wote waliojitokeza kuunga mkono katika Jambo hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa letu wakiwemo Viongozi wetu ndani na nje ya Kigamboni, wanahabari, Taasisi Mbali mbali, Makampuni na Jamii kwa Ujumla.
Tunakaribisha Ushiriki/ Udhamini wa Makampuni mbali mbali kutoka ndani na nje ya Kigamboni na kunatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni kuitumia fursa hii kujumuika pamoja na kuonyesha walichonacho lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.
Muandaaji wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Kigamboni Dimo Debwe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kutambulisha Mbio hizo zitakazo fanyika Desemba 2 Mwaka hu kuanzia eneo la Fun City Mpaka Daraja la Kigamboni.
Mmoja wa Wafadhili wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa, Sunil Rodrigues akieleza kwanini mbio hizo zitafanyika katika eneo la Fun City Kigamboni.
Mratibu wa Masuala ya Habari wa Mbio za Kigamboni, mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya ushiriki wa Wanahabari Kumi katika Mashindano hayo.
Uongozi wa Mashindano ya Riadha ya Kigamboni Marathoni wakionyesha Flana zitakazotumika katika Mbio za Kigamboni Intenational Marathon.
No comments:
Post a Comment