Thursday, October 4, 2018

DKT.CHAULA:HAKIKISHENI VITUO VYA AFYA VYOTE NCHINI VINA HATI MILIKINaibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.
Jengo la Wodi ya wazazi lililopo katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula akikagua ukarabati na ujenzi wa chumba cha upasuaji na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid Mchatta (katikati) wakikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI KIGOMA


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula amewaagiza viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha vituo vyote vya afya vinapatiwa hati miliki.

Dkt. Chaula ameyasema hayo alipokuwa akikagua ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya cha Mabamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini leo Mkoani Kigoma.

Amesema kuwa Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya afya nchini, hivyo Mamlaka za Serikali za Mitaa hazinabudi kuhakikisha zahanati na vituo vyote vya afya nchini vinakuwa na hati miliki.

“Viongozi wamekuwa wakitoa maagizo kuhusu uwepo wa hati miliki kwa majengo ya Serikali lakini bado baadhi ya watendaji wa Mamlaka husika hawatekelezi maagizo hayo, hivyo nawaagiza viongozi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kila Zahanati, Kituo cha afya kinakuwa na Hati Miliki.” Anasisitiza Dkt. Chaula.

Akiongelea kuhusu ukusanyaji wa mapato Dkt. Chaula amesema kuwa kila kituo cha afya kinatakiwa kufunga mifumo ya kielektroniki ili kuongeza mapato kwenye vituo vya afya.“Sijaridhishwa na hali ya ukusanyaji wa mapato katika Zahanati na vituo vya afya kwa kuwa mapato bado nimadogo ukilinganisha na huduma zinazotolewa ukizingatia kuwa Serikali imeweza kukarabati na kujenga miundombinu ya afya nchini, hivyo nawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato katika vituo hivyo” Anasema Dkt. Chaula

Naye Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo Dkt.Sebastian Pima amesema kuwa ujenzi na ukarabati wa awamu ya kwanza umetekelezwa katika kituo cha Afya cha Mabamba na kugharimu shilingi milioni 500.Dkt. Pima ameyataja majengo yaliyojengwa kuwa ni wodi ya kinamama yenye uwezo wa kuchukua vitanda vine (4), Kliniki ya baba, mama na mtoto, nyumba ya mtumishi, chumba cha kuifadhia maiti, chumba cha upasuaji, chumba cha kufulia, maabara na ukarabati wa jengo lazamani la wodi ya wazazi.

Aidha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Zainabu Chaula yupo kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya nchini na tayari ameshatembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.

No comments: