Saturday, July 14, 2018

PADRI AUGUSTINO RAMADHAN AONGOZA IBADA YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA MKE WA PROFESA SHABA

 Padri wa Kanisa la Anglikana, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Elizabeth Shaba mke wa Profesa James Shaba aliye patwa na mauti Julai Mosi mwaka huu na kuzikwa Julai 7, Chicago, Marekani. Ibada hiyo imefanyika leo kwenye Kanisa la St Albano Angilkana, jijini Dar es Salaam.

Marehemu ambaye alikuwa anaishi na mumewe nchini Marekani mpaka anakutwa na mauti alikuwa Muuguzi Mshauri wa Ubalozi wa Kanada. Alioana na Profesa Shaba mwaka 1963. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
 Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakishiriki kwenye Ibada hiyo
 Anna Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere, akishiriki katika Ibada hiyo
 Wakiimba wimbo wakati wa ibada


 Wakishiriki kutoa sadaka wakati wa ibada hiyo


 Ndugu wa marehemu Elizabeth Shaba, Grace Shaba akitoa sadaka




 Padri Augustino Ramadhan akiwapatia waumini chakula cha bwana
 Wakishiriki kumuombea marehemu Elizabeth Shaba
 Charles Shaba ambaye ni mmoja wa viongozi wa familia akielezea wasifu wa marehemu Elizabeth Shaba

 Baadhi ya wanafamiia wakiwa katika picha ya pamoja
 Wakipata chakula cha mchana baada ya ibada kumalizika

No comments: