Saturday, June 16, 2018

WAZIRI JAFO ATANGAZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

Mhe. Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya Sanaa na biashara.Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Mhe. Jafo alisema jumla ya wanafunzi 11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)

Aliagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2018 wahakikishe wanaripoti katika shule zao kuanzia tarehe 15,Julai,2018 na atakayechelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.

Mhe. Jafo alisistiza kuwa uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya ufundi umefanyika kwa kuzingatia ufaulu na nafasi zilizopo katika shule, hakutakuwa na fursa ya kufanya mabadiliko yeyoye ya shule kutokana na ukosefu wa nafasi kwenye shule husika.

Alisema wanafunzi waliopangwa kwenye vyuo vya kati wanapaswa kudhibitisha kukubali kujiunga na kozi walizochaguliwa hadi ifikapo 8 Agosti, 2018 ili kuthibitisha kuwa wamekubali kozi na vyuo walivyopangiwa kwa wanafunzi watakaoshindwa kuthibitisha nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine.

Amewapongeza walimu, wazazi na wakezi kwa juhudi walizozifanya katika ufundishaji na kuwezesha wanafunzi kufaulu vizuri na kuwaagiza kuendelea kusimamia na kufuatilia maendeleo ya watoto nchini.Aidha ametoa wito kwa Wakuuwa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji kuhakikisha azima ya Serikali ya kila Tarafa kuwa na shule ya Kidato cha Tano inatekelezwa ili kuwezesha wanafunzi wote wanaofaulu Kidato cha Nne kuapata na fasi ya kuendelea na masomo ya kidato cha 5 na 6.

“Mikoa ihakikishe inakuwa na tahasusi zote za msingi katika shule zake ili kuwapunguzia wazazi gharama za usafiri kwenda shule za mbali nje ya Mkoa” Alisema Jafo.Aidha amesema kutokana na ongezeko la ufaulu wa masomo ya Sayansi kila shule zinazoanzishwa kuhakikisha zinajengwa maabara ili kuongeza idadi ya wanafunzi wa tahasusi za Sayansia ambao ufaulu wao umekuwa ukiimarika kila mwaka.

No comments: