WAKINA mama 925,342 nchini wamefanikiwa kusajiliwa na mradi wa “Tumaini
la Mama tokea ulipoanza mwaka 2012 na kuweza kunufaika huduma
zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Mbaruku Mgawa wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa
mradi wa “Tumaini la mama kwa viongozi na watendaji mkoani Tanga
kilichofanyika mjini Korogwe.
Alisema idadi hiyo ni kuanzia mpango huo ulipoanza hadi mwezi Mei mwaka
huu huku wakina mama wapatao 323,797 wakitokea mkoani Tanga pekee ambao
wamesajiliwa.
Aidha alisema pia kaya 323.797 zimenufaika na kulipiwa fedha kwa ajili
ya kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo sh.milioni
48,077,859,434 zimelipwa kwa watoa tokea mradi huo ulipoanza huku vituo
vya mkoa wa Tanga vikilipwa kiasi cha sh.milioni 12,449,902,412.
“Pia vifaa tiba vyenye ya sh. milioni 900 vimenunuliwa na kusambazwa
katika vituo vya kutolea huduma pia mradi umesaidia upatikanaji wa
computers katika vituo vyenye mahitaji kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa
kumbukumbu”Alisema.
“Kwa kuzingatia mafanikio yaliyopatikana mfuko utakaa na mfadhili kuona
uwezekano wa kupata fedha zaidi kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma kwa
wananchi sisi viongozi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba mradi
unatekelezwa kama ilivyokusudiwa ili mfadhili aone umuhimu wa kuongeza
muda zaidi”Alisema.
Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella alisema hatua ya mfuko huo kubuni mpango huo umekuwa ni
mkombozi mkubwa kwa wakazi wa mkoa huo na hasa wakima mama ambao sasa
wana uhakika wa kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya
bila gharama zozote.
Alisema mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya watu kupitia
mpango huo wa Tumaini la Mama ambapo takribani wakina mama 323,797
wamenufaika na mradi huo ambao ni muhimu kwao.
“Lakini kabla ya kuanza kwa mradi huu mwaka 2012 idadi ya wanawake
waliokuwa wanajifungulia katika vituo vya matibabu haikuwa kubwa
kutokana na sabab u mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa elimu juu ya
umuhimu wa uzazi salama pamoja na afya ya uzazi”Alisema
“Pamoja na gharama ya uzazi kuwa juu, kukosekana kwa huduma bora katika
vituo vya kutolea huduma hasa upungufu wa dawa, vifaa pamoja na
miundombinu isiyokuwa rafiki kwa ajili ya afya ya Mama na Mtoto”Alisema
Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa kuwa lengo kuu la mradi ni kupunguza vifo
vya mama na mtoto kwa kuhakikisha kwamba akina mama wote wanajifungulia
katika vituo na wanapata huduma bora.
Aliongeza kuwa hivyo mradi huo unatoa fursa kwa mama mjamzito kupata
kadi ya Bima ya Afya kwa ajili ya kupata huduma za afya katika kipindi
cha ujauzito na miezi sitaa baada ya kujifungua yeye na mtoto
aliyezaliwa ikiwemo familia ya mama mjamzito yenye idadi ya watu
wasiozidi sita wanalipiwa fedha kwa ajili ya kujiunga na mfuko wa Afya
ya Jamii kwa mwaka mmoja katika halmashauri yake.
No comments:
Post a Comment