Friday, June 22, 2018

ROSE MBAGA ATAKA WATANZANIA KUSAIDIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA AJIRA KWA VIJANA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWEZESHAJI wa Vijana katika masuala ya maendeleo endelevu nchini Rose Mbaga amesema ikitokea akapata nafasi ya kukutana na Rais Dk.John Magufuli atamuelezea kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana nchini.

Pia amesema katika kutatua changamoto ya ajira ametoa rai kwa Watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kuitatua huku akisisitiza ipo haja kwa vijana kuwa na uthubutu wa kufanya mambo yanayohusu maendeleo.

Mbaga ametoa kauli hiyo jana usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akijiandaa na safari ya kwenda  nchini Uingereza baada ya kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine kwenye kazi za kijamii .Akiwa huko atakabidhiwa tuzo ya STAR AWARD.

"Ikitokea siku nikapata nafasi ya kukutana na Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kikubwa nitakachomwambia ni kuhusu kuwasadia vijana na hasa wanaohitimu elimu ya juu.

"Kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanahitimu elimu ya juu na changamoto yao kubwa ni ajira.Hivyo namatamani kumwambia umuhimu wa kukutana na vijana na kisha kwa pamoja tujadiliane namna ya kutatua changamoto hiyo,"amesma Mbaga.

Pia Mwanadad huyo ambaye amekuwa akijihusisha na kuhamasisha makundi ya rika mbalimbali yakiwamo ya vijana amesema anaamini kuthubutu ni jambo muhimu na hata yeye amefika hapo kwasababu ya kuthubutu na kutoa mchango wake kwa ajili ya nchi yake na nchi nyingine mbalimbali duniani.

Ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuhakikisha wanashiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kufafanua baada ya kumaliza chuo mwaka 2010 alikaa nyumbani kwa miaka mitatu na baadae aliamua kuanza kufanya kazi za kujitolea na sasa amekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine

Alipolizwa amewafikia watu wangapi hadi sasa katika kuhamasisha kushiriki kufanya maendeleo na amesema amekutana na maelfu ya watu wakiwamo vijana wa Tanzania na mataifa mengine duniani.

Akiwa uwanjani hapo akijiandaa kusafiri kwenda Uingereza Mbaga amesema anakwenda katika nchi hiyo kwa ajili ya kupata tuzo maalumu ya kutambua mchango wake na yumo kwenye kundi la wanawake 100 duniani ambao wameonekana kuwa na mcahngo mkubwa wa kuhamasisha maendeleo.

Akizungumzia baadhi ya tuzo ambazo amezipata amesema mwaka 2017 alipata tuzo ya "African youth empowerment" chini ya Africa Youth Awards .Amefafanua kwa sasa ni Rais wa World Merit Tanzania chini ya Shirika la World Merit lililopo Uiengereza.

Amesema shirika hilo limejikita katika kuhamasisha Maendeleo endelevu na kfafanua mwaka 2016 alipata nafasi ya kuhudhuri moja ya program za shirika hilo iliyokuwa inaitwa Merit360."Kupitia programu hiyo niliweze kuhamasisha umuhimu wa mazingira Umoja wa Mataifa na kushinda "Sustainable development goals challenge competition" .

"Na nilifanikiwa kuwafikia watu zaidi ya 1000 kujua umuhimu wa mazingira  nchini Tanzania,"amesema Mbaga.Pia amesema safari yake kwenye masuala ya maendeleo ilianza kwa kujitolea kupitia mashirika mbalimbali kwa miaka  mitatu.
"Baadhi ya tuzo nyingine niliyoipata ni ya "Woman of Influence in events hall of fame chini ya Association for women in event ya Marekani 2017.

"Na mwaka huu nchini Uingereza nimeweza kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine Kwenye Kazi za kijamii Kama STAR AWARD,"amesema Mbaga.

No comments: