Video
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea
kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba
Swagaswaga.
Na Hamza Temba-WMU-Chemba, Dodoma
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi
waliovamia Pori la Akiba Swagaswaga na kuendesha shughuli zao ikiwemo kilimo,
makazi na ufugaji ndani ya pori hilo kinyume cha Sheria waondoke mara moja kwa hiari yao kabla ya
kuondolewa kwa nguvu.
Ametoa
agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Handa Wilaya ya
Chemba mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua mgogoro wa ardhi
kwenye hifadhi hiyo wilayani humo.
"Tunawapa
siku 30 muanze kutoka wenyewe, baada ya siku 30 tunatoa notisi ya siku nyingine
30 za kutumia nguvu, kwahiyo kuanzia sasa hivi anzeni kujipanga wenyewe na
kuondoka wakati Halmashauri ikifanya tathmini ya maeneo ya vijiji ambavyo ni
halali ya kuwagawia kwa wale watakaopenda kupewa maeneo huko", alisisitiza
Dk. Kigwangalla.
Alisema
sheria za uhifadhi haziruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya maeneo ya hifadhi na
kuendesha shughuli za kibinadamu na kwamba kufanya hivyo ni kudharau Sheria na
Malmlaka zilizopo.
Alisema
kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Handa ambacho kilianzishwa kimakosa ndani
ya pori hilo wataendelea kubaki mpaka pale wizara yake kwa kushirikiana na
Wizara ya Tamisemi na Ardhi zitakapoamua hatma yao ikiwemo ama kulipwa fidia
kupisha eneo hilo au waendelee kubaki na mipaka ya hifadhi isogezwe.
Katika
hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania TAWA kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka katika chemchem iliyopo
ndani ya hifadhi hiyo na kuyasogeza kwenye makazi ya wananchi ili kulinda chanzo
hicho kwa kuzuia uharibifu unaofanywa na wananchi wanaofuata huduma katika eneo
hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga alisema atasimamia ipasavyo maagizo
yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla na kwamba endapo wanavamizi hao walioingia
ndani ya pori hilo kinyume cha sheria watakaidi agizo hilo atatoa notisi ya
siku 30 na hatimaye kuwaondoa kwa nguvu ili kupisha eneo hilo liendelee
kuhifadhiwa.
Kwa
upande wake mbunge wa Chemba, Juma Nkamia alimshukuru Dk. Kigwangalla kwa
kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo na kuwataka
wananchi kutii sheria na kuepuka kuvamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria ili
kuepuka usumbufu na mamlaka zinazosimamia eneo hilo.
Viongozi
wengine walioongozana na Dk. Kigwangalla katika utatuzi wa mgogoro huo ni
Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson
Masaka, na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa wilaya za Chemba na
Mkalama.
Kijiji
cha Handa kilisajiliwa tarehe 16 Agosti, 2004 kikiwa na ukubwa kilomita za
mraba 72.23 na vitongoji vitano, vinne kati yake vikiwa ndani ya Pori la Akiba
Swagaswaga. Vitongoji hivyo ambavyo ni Ilala A, Ilala B, Mbugani na Mnang'ana
vina ukubwa wa kilomita za mraba 7.85 na kaya 1,169 zenye watu zaidi ya
5,291.
Pori
la Akiba Swagaswaga lilianzishwa kwa Tangazo la Serikali namba 72 la tarehe 21
Februari, 1997 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 871. Pori hilo lipo katika
wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma na wilaya ya Singida Vijijini mkoani
Singida.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia akizungumza katika mkutano huo katika kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma
wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla
alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori
la Akiba Swagaswaga.
Mbunge wa Hanan'g, Dk. Marry Nagu akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya
Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina
mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya
Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia,
Mbunge wa Hanang, Dk. Marry Nagu, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga, Mkuu
wa Wilaya ya Mkalama, Mhandisi Jackson Masaka, na viongozi wengine wa wilaya ya
Chemba na Mkalama wakiangalia ramani ya mpaka Pori wa Pori la Akiba Swagaswaga
alipotembelea eneo hilo jana kwa ajili kutatua mgogoro wa hifadhi na vijiji.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na viongozi wengine wa wilaya ya
Chemba na Mkalama wakikagua mpaka wa Pori la Akiba Swagaswaga ambalo lina
mgogoro na kijiji cha Handa alipotembelea eneo hilo jana katika wilaya ya
Chemba mkoani Dodoma kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla alipotembelea kijiji hicho jana kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
No comments:
Post a Comment