Saturday, June 23, 2018

KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA

KAMPUNI ya Aon kupitia Minet imezindua rasmi JH Minet Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa safari iliyoanza 1998 ikiwa inatoa huduma za bima pamoja na mafao.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Minet Group Joe Onsando amesema kuwa kampuni hiyo mpya itakuwa chini Aon na hakuna kazi itakayopotezwa baada ya mabadiliko hayo.

Amesema  kuwa Minet  ni kampuni inayoaminika  kote Afrika na nje ya bara hilo na wafanyakazi wa Aon ambayo sasa itajukulikana Minet katika nchi hizo na viongozi wao ambao wana ujuzi katika masuala ya viwanda wataendelea kuwa nafasi kama watendaji katika utoaji wa huduma.Onsando ameeleza kuwa mwaka 1997  kampuni hiyo ya  JH Minet ilibadilishwa na kuwa Aon Minet na wanaendelea kujenga uchumi imara Afrika na itaendelea kuwa sehemu ya Aon katika utendaji kazi wao.

Onsando amefafanua kuwa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo hazitabadilika katika sekta zote kama vile kilimo, madini na mawasiliano.Pia amesema wanafurahishwa na namna uwekezaji unavyoendelea na kukua barani Afrika na wataendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa sasa na baadaye.

Naye Mkurugenzi wa JH Minet Tanzania Raju Dave ameeleza kuwa Tanzania kama sehemu nzuri ya biashara imeendelea kukua kiuchumi Mashariki mwa Afrika ukilinganisha na miaka ya nyuma.Na amehaidi kuendeleza ukuaji wa uchumi kupitia gunduzi mbalimbali katika sekta mbalimbali na amehaidi huduma bora kwa wateja.

Kwa mujibu wa uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa uzinduzi wa jina hilo la Minet ni awamu ya pili ya muendelezo wa kufanya mabadiliko hayo ambapo tayari nchi nyingine kadhaa barani Afrika wameshabidili jina.Pia uongozi umesema unafurahishwa na namna ambavyo Serikali ya Tanzania inavyojikita katika kuimarisha uchumi.

Wamesema mwenendo wa hali ya nchini nchini Tanzania inafurahishwa na inavutia kwa kampuni nyingine ikiwemo ya kwao kuwekeza nchini katika masuala yanayohusu shughuli za bima na mafao.Kwa upande wake mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka amesema utulivu uliopo katika bara la Afrika unatosha kuwafanya waafrika kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.

Viongozi wa kampuni ya Minet wakizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa kufanya mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.

Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. 
Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania. 

Mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka akisakata rumba na baadhi ya wageni waalikwa kwenye tukio la uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET.

No comments: