Tuesday, June 12, 2018

MAHAKAMA YATUPILIA MBALI OMBI LA UPANDE WA UTETEZI KESI YA AKINA MBOWE, WENZAKE

Na Karama Kenyunko, blogu ya jami

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la upande wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema na wenzake saba lililokuwa linatoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi mdogo uliotolewa mahakamani hapo jana.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka Juni 11mwaka 2018 kuamuriwa na Mahakama wafanye marekebisho katika hati ya mashtaka baada dhidi ya washtakiwa hao badaa ya hati hiyo, kuonekana kuwa na mashtaka batili na yenye mapungufu ya kisheria.

Kutokana na kutupwa kwa kusudio hilo la kukata rufaa, washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mapya 13 na na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba John Mnyika.

Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Katika mashtaka hayo mapya yaliyofanyiwa marekebisho, imedaiwa washtakiwa hao, kwa pamoja Februari 1 na 16 mwaka 2018, Dar es Salaam washtakiwa pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.

Pia imedaiwa, siku hiyo katika viwanja vya buibui na Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na adhma ya pamoja, waliitekeleza adhma yao kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea uvunjïfu wa amani.

Pia watuhumiwa hao wanadaiwa kutekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuleta hofu ya uvunjifu wa amani.

Wakili Nchimbi alidai watuhumiwa hao walikaidi tamko lililowataka kutawanyika lililotolewa na Ofisa wa Polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani uliopeĺekea hofu na hatimaye kifo cha Akwilina na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.Pia Mbowe anadaiwa, siku na mahali hapo, wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo la Kinondoni katika mkutano wa adhara alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi yalikuwa na lengo la kuamsha hisia za chuki miongoni mwa watanzania.

Pia Mbowe anadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika mkutano wa umma uliofanyika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Mbowe alitamka maneno mabaya yaliyokuwa na nia ya kuinua hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya serikali halali iliyopo madarakani

Mshtakiwa Mdee anadaiwa , siku hiyo, akiwahutubia wakazi wa Kinondoni alitamka maneno yaliyokuwa na lengo kuhamasisha hisia za chuki miongoni mwa watanzania.Kwa upande wa Heche anadaiwa kuwa kutamka maneno yaliyokuwa na lengo kuamsha hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya utawala uĺiopo madarakani.

Mshtakia Mbowe katika shtaka jingine anadaiwa kutoa maneno yaliyokuwa na na nia ya kuleta chuki na hali ya manung'uniko miongoni mwa jamii dhidi ya utawala ulïopo madarakani.Pia Mbowe anadaiwa kutoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau kwa upande wa raia wa Tanzania dhidi ya mamlaka halali kuwa "Hii nchi Aidha anadaiwa kuwashawishi wakazi wa Kinondoni kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio halali.

Katika shtaka jingine, mshtakiwa Msigwa anadaiwa kushawishi raia na wakazi wa eneo hilo kutenda kosa la jinai kwa kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.Aidha, Bulaya anadaiwa kutenda kosa la kukaidi amri halali ya tamko.

Washtakiwa wamekana mashtaka hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 18, mwaka huu.

No comments: