Sunday, June 10, 2018

MAFUNZO YA WISN NA POA YALIYOSHIRIKISHA MIKOA MINNE YAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO.

Na Andrew Chimesela, Morogoro

Mafunzo ya kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo unaojulikana kwa jina la kitaalamu Workload Indicators of Staffing Needs - WISN na Prioritaization and Optimization analysis – POA (WISN plus POA)  yaliyoanza Juni 4 mwaka huu katika ukumbi wa ICE wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne – SUA Mkoani Morogoro yamehitimishwa Juni 8 kwa mafanikio makubwa.
Akiongea na washiriki wenzake wakati wa Kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu  Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja amewapongeza wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kujitahidi kuwapa kile walicholenga kutoa hadi wao kuelewa  kwa ufanisi na kwa niaba ya wenzake ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika Halmashauri zao.
Bw. Masanja ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo amewataka washiriki wenzake kutambua kuwa hadi sasa watumishi wa Serikali hususan wa kada ya Afya bado hawatoshelezi kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo ni wajibu wao kutumia mafunzo waliyoyapata kuisaidia Serikali kuwapanga vizuri watumishi waliopo kulingana na uzinto wa kazi.
“Washiriki wenzangu, tumeshajifunza kuwa kituo cha Afya kilichopo Mjini hakiwezi kulingana majukumu yake na uzito wake wa kazi na kituo cha Afya cha kijijini, kwa sababu hata idadi ya wagonjwa inatofautiana, kwa hiyo tuisaidie Serikali kuondoa malalamiko  kwa kuwapanga vizuri watumishi waliopo kulingana na uzito wa kazi zinazopatikana kwenye maeneo husika” alisema Bw. Masanja.
Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha upangaji wa watumishi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kulingana na Uzito wa kazi, kwa kutumia Mfumo wa kisayansi wa WISN PLUS POA na kushirikisha Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Mikoa minne ambayo kwa kituo cha Mkoa wa Morogoro kilijumuisha Mikoa ya  Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na Arusha.
Haya ni mafunzo yanayofadhiriwa na Mradi wa uimarishaji mifumo katika  Sekta ya Umma (Public Sector  System Strenthening - PS3) na kuratibiwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, wawakilishi kutoka Halmashauri na taasisi ya Touch Foundation na yanatolewa kwa Wataalamu wa sekta ya Afya kwa Halmashauri za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\PS 3 web\DSCN1813.JPG
Bw. Renatus Mashauri  ni mtoa mada ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Rasilimali watu -  mradi wa PS3
Happines Ndosi - Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji  - Ifakara.
Solomon Dktari Kibaha, Mtoa mada.
Mratibu wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma (PS3) Mkoa wa Morogoro Bw. David Laput.

C:\Users\CHIMESELA\Desktop\PS 3 web\DSCN1809.JPG
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\PS 3 web\DSCN1863.JPG
Wataalamu wa Sekta ya Afya walioshiriki mafunzo ya WISN na POA yaliyoratibiwa na kufadhiliwa na PS3 na kufanyika katika ukumbi wa ICE katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA Mjini Morogoro.
Baadhi ya timu ya  viongoi wa mafunzo ya WISN PLUS POA wakiwa tayari kukabidhi vitabu vilivyoandaliwa kwa ajili ya kutekeleza kile walichojifunza washiriki wa mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Gracian Makota, Renatus Mashauri na Bw. Sebastian Masanja. Wengine ni wenyekiti wa washiriki wakati wa mafunzo na David Laput Mratibu wa PS 3 Mkoa wa Morogoro.

Bw. Sebastian Masanja ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala, Mkoa wa Kilimanjaro aliyefunga mafunzo hayo akimkabidhi vitabu Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya WISN PLUS POA SUA Mkoani Morogoro.  
DSCN1936
Mgeni Ramsi aliyefungua mafunzo ya WISN PLUS POA Dkt. Frank Jacob (katikati waliokaa) ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mikoa ya Morogoro na Dodoma yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA.
C:\Users\CHIMESELA\Desktop\DSCN3786.JPG
Mgeni Ramsi aliyefungua mafunzo ya upangaji wa watumishi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kulingana na Uzito (WISN plus POA) kwa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro Bw. Noel Kazimoto (katikati waliokaa) ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA.




No comments: