Sunday, June 10, 2018

ELIMU BORA KUIWEZESHA TANZANIA KUPIGA HATUA YA UCHUMI WA VIWANDA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia) , wakiwasili katika viwanja vya Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, mkoani Dodoma, kushiriki tukio la uzinduzi wa Kambi ya masomo ya wanafunzi 442 wa Kidato cha Pili na cha Nne kutoka shule za sekondari 23 za wilaya ya Kondoa, wanaojiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Wanafunzi 442 wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao, wakiwa katika kambi katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa ikiwa ni mkakati wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji wa kuinua kiwango cha ufaulu na elimu wilayani humo ambapo mfuko wake wa Jimbo umetumia zaidi ya shilingi milioni 90 kufanikisha makambi hayo katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Kidato cha Pili na cha Nne wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi ya kambi ya masomo katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Kidato cha Pili na cha Nne wa shule za Sekondari katika wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi katika shule zao wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi ya kambi ya masomo katika Shule ye Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko kata ya Pahi, Wilayani Kondoa, kujiandaa na mitihani yao ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Bi. Sezaria Makota, akielezea namna wilaya yake ilivyopiga hatua kubwa kielimu kufuatia hatua ya Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 90 za Mfuko wa Jimbo katika Sekta ya Elimu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuboresha elimu nchini baada ya kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na uamuazi wake wa kutumia zaidi ya asilimia 80 ya Mfuko wake wa Jimbo kuwekeza katika elimu kwa kuwa ndicho kipaumbele chake cha kwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuboresha elimu nchini baada ya kuamua kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari na uamuazi wake wa kutumia zaidi ya asilimia 80 ya Mfuko wake wa Jimbo kuwekeza katika elimu kwa kuwa ndicho kipaumbele chake cha kwanza.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge (wa sita kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (Mb), Dkt. Ashatu Kijaji (wa tano kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Sekondari waliojitolea kuwafundisha wanafunzi 442 wanaoshiriki kambi maalumu kwa ajili ya kujiandaa na mitahani yao ya kitaifa, katika shule ya Sekondari Amani Abeid Karume, iliyoko Kata ya Pahi, Wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, mkoani Dodoma, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota, wakipongezana baada ya kufanikisha uzinduzi wa kambi maalumu ya wanafunzi wa kitado cha Pili na cha Nne kutoka shule 23 za Sekondari wilayani Kondoa, mkoani humo, mpango uliofanikisha kuongeza kiwango cha ufaulu wilayani humo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Benny Mwaipaja, WFM, Kondoa

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa uwekezaji katika elimu bora kwa vijana wa kike na wa kiume kutaiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati wa viwanda hata kabla ya mwaka 2025.

Dokta Kijaji ameyasema hayo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa kambi inayowahusisha wanafunzi 260 wa kidato cha pili na cha nne kutoka shule 23 za Sekondari wilayani humo wanaopatiwa mafunzo ya kina ili kujiandaa na mitihani yao.

Kambi hiyo inafanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo ambapo kiasi cha shilingi milioni 90 za mfuko wa Jimbo la Kondoa zimetumika na kuiwezesha wilaya hiyo kupanda daraja kielimu kutoka nafasi za mwisho kitaifa hadi kufikia nafasi za juu kabisa.

“Athari chanya ambayo ninataka kuiacha Kondoa ni elimu bora kwa vijana wetu inayokwenda sambamba na uamuzi wa Mhe. Rais wetu Dkt. Jihn Magufuli, wa kutoa elimu ya msingi na Sekondari bure kwa wanafunzi hivyo kuongeza thamani ya uamuzi huo wa Serikali” Alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa baada ya hatua ya Halmashauri ya wilaya hiyo kutoa mtihani wa aina moja wa majaribio kwa shule za msingi na kuonesha mafanikio makubwa, hatua hiyo sasa itaelekezwa kwenye elimu ya Sekondari ili kuwapima vyema wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao ya kitaifa.

Akizungumza kabla ya kuzindua kambi hiyo ya siku 25, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, amesema kuwa taifa lenye wasomi waliobobea katika nyanja mbalimbali wataisaidia nchi kukabiliana na mikataba mibovu inayo pora rasilimali za nchi.

Aliwataka wanafunzi hao kutumia vizuri fursa waliyoipata kwa kusoma kwa bidii na maarifa ili waje kulitumikia taifa ili liweze kufikia maendeleo ya haraka kwa kuhakikisha kuwa wanalinda kwa nguvu zao zote rasilimali hizo za Taifa yakiwemo madini, gesi na mazingira.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota, amempongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Dkt. Ashatu Kijaji, kwa kusimamia kidete suala la elimu ya watoto wa wilaya yake kupitia mfuko wa jimbo, hatua iliyoifanya wilaya hiyo kupata tuzo mbalimbali za ubora wa elimu katika kipindi cha miaka mitatu

No comments: