Sunday, June 10, 2018

JULIO ASEMA, UWEZO WA ALI KIBA SIO WA NCHI HII.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kocha Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa uwezo wa kimpira wa msanii Ali Saleh Kiba ni wa kucheza soka la kulipwa la kimataifa nje ya nchi.

Hayo aliyasema baada ya kumalizika kwa mchezo wa hisani wa kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundi mbinu mashuleni uliopewa jina la NIFUATE baina ya Marafiki wa Ali kiba na Marafiki wa Mbwana Samatta.

Julio amesema kuwa, uwezo wa Ali Kiba ni mkubwa sana na mara nyingi amekuwa anamuomba amsajili katika timu anazofundisha ila mwenyewe hakuwa tayari kucheza soka la ushindani.

"Mara nyingu nimekuwa namuomba nimsajili katika timu nazofundisha na nikiwa namwambia kabisa kuwa asije mikoani kucheza ila timu inapokua inakuja Kucheza Dar es salaam atakua anacheza," amesema Julio.

Amesema kuwa anachokifanya Ali Kiba uwanjani ni kikubwa zaidi kuliko wachezaji wanaopewa hela nyingi katika timu za Yanga na Simba."Ali kiba kama anaamua kucheza soka la ushindani ndani ya mwaka mmoja basi mwaka unaofuata lazima akacheze nje maana ana uwezo mkubwa sana ila soka letu nchini haliangalii vitu kama hivi,"

Julio," naweza kusema Ali Kiba ni aina ya mchezaji ambaye akikaa na mwalimu anayejua mpira kama mimi basi anaweza akafanya maajabu makubwa sana uwanjani, uwezo wake sio wa kucheza soka la hapa nchini".

Ali kiba amekuwa moja ya wasanii wanaolisakata kabumbu kwa uwezo wa hali ya juu lakini akiwa hapendelei kucheza soka la ushindani na watu wengi wakiwa wanatamani kumuona akicheza mchezo huo katika moja ya timu za ligi kuu nchini.

Lakini kwa upande wake Ali Kiba aliweka wazi msimamo kuwa kati ya mpira na muziki aliamua kuchagua muziki na kuachana na soka la ushindani ila bado anacheza katika mechi mbalimbali za kirafiki na hata mashindano yasiyokua makubwa kwani mpira ni kipaji chakd kingine.

Ali Kiba na Mbwana Samatta waliandaa mchezo wa hisani sambamba na marafiki zao kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazosaidia kukarabati miundi mbinu ya shule za Msingi kila mmoja akianzia katika shule aliyosoma ambapo waliamua kuweka kiingilio ambacho watanzania wengi wangeweza kukidumu cha shillingi 2000 viti vya kawaida na 3000 kwa VIP.

Kwenye mchezo huo pia uliweza kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe huku kwa upande wa Ali Kiba akiambatana na familia yake wakiongozwa na mama yake mzazi na Samatta wakiongozwa na Baba yake Mzee Ally Samatta.

No comments: