Sunday, June 10, 2018

TEAM SAMATTA YAIKANDAMIZA TEAM KIBA MAGOLI 4-2 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Samatta na Mchezaji wa Timu ya Genk ya Ubeligiji Mbwana Samata katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda  cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Samatta na Mchezaji wa Timu ya Genk ya Ubeligiji Mbwana Samata katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda  cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Kiba na Mwanamuziki Ali Kiba kwenye mchezo wa hisani uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa kati ya timu ya mwanamuziki Ali Kiba na Mbwana Samata Mchezaji wa timu ya Genk ya Ubeligiji.
 Kikosi cha timu ya Mwanamuziki Ali Kiba  kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo.
 Kikosi cha timu ya mchezaji wa timu ya Genk ya Ubeligiji Mbwana Samatta kikiwa katika picha ya pamoja.
 Nchezaji wa timu ya Ali Kiba Ibrahim Ajib akikokota mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Mbwana Samatta wakati mchezo huo ukiendelea.

 Mchezaji Hassan Kessy wa timu ya Mbwana Samatta akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Ali Kiba.

 Mbwana Samatta akimiliki mpira ili kutengeneza pasi huku mchezaji wa timu ya Ali Kiba wakati mchezo huo ukiendelea.

 Wachezaji wa timu ya Ali Kiba wakitoka uwanjani mara baada ya kupulizwa filimbi kipindi cha mapumziko.

 Wachezaji Thomas Ulimwengu wa Timu ya Mbwana Samatta kushoto  na Uhuru Selemani wa timu ya Ali Kiba wakitoka nje ya uwanja wakati wa kipindi cha mapumiziko.
Mchezaji Mbwana Samatta akitoka nje ya uwanja huku akizungumza na mmoja wa wapiga picha wakati wa kipindi cha mapumziko.

No comments: