Friday, June 29, 2018

KATIBU MKUU WA CCM BASHIRU ALLY AMTAKA MFANYABIASHARA JIJINI DODOMA KUREJESHA ENEO LA CCM ANALODAIWA KULIHODHI KWA MIAKA MINGI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dk. Bashiru Ally amemtaka mfanyabiasha aliyetajwa kwa jina moja la Deogratius wa jijini hapa, kurejesha kwa hiari yake eneo la CCM ambalo anadaiwa kulihodhi kwa miaka kadhaa sasa katika Kata  ya Makutupola wilaya ya Dodoma Mjini ambalo amekujenga ukumbi na fremu kadhaa za maduka.
Dk. Bashiru ametoa agizo hilo kwa mfanya biashara huyo leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika Kata ya Nakutupola jijini hapa.Amesema amefikia uamuzi huo kwa sababu mfanyabiashara huyo ameonekana kutokuwa na uaminifu wa kutosha kwa kuwa hivi karibuni alizungumza nae ofisini kwake na kuahidi kukutana ili kufanya makabidhiano ya eneo hilo kwa sherehe na nderemo kwenye kikao hicho.

"Cha kushangaza juzi akikuja mwenyewe ofisini kwangu tukaxungumza kwa muda wa saa mbili tukakubaliana leo aje kwenye kikao hiki kukabidhi eneo letu kwa sherehe na ndelemo lakini leo nimempigia hadi simu akasema eti ameenda Dar es Salaam kushughulika na masuala ya mwanae, sasa  endeleeni na mazungumzo  na utaratibu wa makabidhiano akabidhi kwa hiari eneo letu", alisema Dk Bashiru

Dk. Bashiru aliwataka wanachama na viongozi wa CCM kutofanya vurugu za aina yoyote kwa Mfanya biashara huyo na kusema Mchakato uliotumika kurejesha ukumbi ndio utakaotumika kurejesha eneo lote la  Chama na mali yote iliyopo kwenye eneo la hilo ni mali ya CCM.

Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally amewapokea Winston Edward Katibu Kata hiyo wa CUF na Baraka Tayara Katibu kata wa Chadema pamoja na wanachama 181 kutoka vyama hivyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akipokelewa na Viongozi mbali mbali alipowasili kata ya Makutupola wilaya ya Dodoma mjini leo.
 Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akiwapungia Mkono kikundi cha ngoma

 Mwenyekiti wa Kata ya Makutu pola akifungua kikao hicho
  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Bi Jamila Yusuph  akizungumza wakati akimkaribisha  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Ndg.Godwin Mkanwa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kuzungumza na Viongozi na wanachama wa Kata ya Makutupola Wilaya ya Dodoma Mjini.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Ndg.Godwin Mkanwa akizungumza wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kuzungumza na Viongozi na wanachama wa Kata ya Makutupola Wilaya ya Dodoma Mjini
 Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM na Jumuiya zake wa Kata ya Makutupola leo
 Katibu kata wa Chadema ndg.Baraka M.Tayara akizungumza mara baada ya kukabidhi kadi yake ya uwanachama toka Chama cha Demokrasia na maendeleo alipoungana na Katibu wa kata hiyo toka CUF Ndg.Winston Edward pamoja na wanachama 181 wa Vyama hivyo Leo walipojiunga na CCM.
 Wanachama na Viongozi wa Chama cha Mpinduzi kata ya Makutupola wakiimba nyimbo ya chama mara baada ya kuwapokea viongozi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na Mwanachama wa CCM mara baada ya mkutano kumalizika( Picha na Fahadi Siraji CCM Blog)

No comments: