Friday, June 29, 2018

Unesco wakabidhi kijiji digitali cha Ololosokwan kwa serikali

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wamekabidhi rasmi kijiji cha digitali cha Ololosokwan katika sherehe kubwa iliyofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Katika kukabidhiana huko Unesco imesema kwamba itaendelea kutoa msaada katika mtandao wa intaneti kwa miezi sita ijayo.
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na Dk. Abdul Rahman Lamin, Ofisa msimamizi wa ofisi ya Unesco, Ann Therese Ndong-Jatta alisema kwamba wakati wanakabidhi facility hizo wamefurahishwa na ushirikiano mkubwa waliopewa katika mradi huo.

Kijiji cha digitali cha Ololosokwan ni moja ya vijiji vinne ambavyo vimefadhiliwa huku vikitoa huduma muhimu za elimu, afya na biashara kuendeshwa kidigitali.Kijiji hicho cha digitali ambacho ni matokeo ya ushirikiano kati ya UNESCO na kampuni ya Samsung imelenga kutoa elimu kwa kutumia njia ya mtandao, kufaniklisha tiba mtandao na pia kutumia mtandao wa kompyuta katika kuwezesha biashara.

Ofisa huyo alisema kuna haja ya kuendeleza ushirikiano uliopo ili mradi uweze kuendelea kuchangia maendeleo ya wakazi wa eneo hilo.
Aidha aliitaka serikali kuhakikisha kwamba inaendeleza ushawishi kwa wananchi wa eneo hilo la Ngorongoro kutumia vyema teknolojia ya kisasa katika kufanikisha maisha endelevu ya zana zilizopo.

“UNESCO inajisikia furaha kwa kutambua kwamba kupitia mradi wa kijiji cha digiti, wilaya ya Ngorongoro imekuwa miongoni mwa waanzizilishi wa matumizi ya Tehama katika kufanikisha elimu na afya nchini Tanzania. “ alisema Ndong-Jatta .Alisisitiza kuwa kuwapo kwa kijiji hicho kunaambatana na mamchakato wa sasa wa serikali ya awamu ya tano ya kuwa na taifa lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Nataka kuhakikishia wilaya ya Ngorongoro, kijiji cha Ololosokwan na serikali ya Tanzania kwamba UNESCO itaendelea kutoa msaada wa kiufundi na kuhakikisha kwamba kunakuwa na maendeleo endelevu kwa kijiji hichi” alisema Ndong-Jatta.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo akizungumza na wananachi wa kijiji cha Ololosokwan pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin akizungumza kwa niaba ya Ann Therese Ndong-Jatta wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu akitoa salamu za Wizara ya Elimu pamoja na za Mbunge  wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na Maendeleo ya Uvuvi, Mh. William Ole Nasha wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkurugenzi wa Tehama MUHAS na Mratibu wa huduma ya tiba mtandao, Dkt. Felix Sukums akitoa salamu za MUHAS wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Diwani wa kata ya Ololoskwan, Mh. Yannick Ndoinyo akitoa neno la shukran kwa niaba ya wananchi wake kwa mgeni rasmi na Unesco kwa ushiriki wao wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Abudl Rahman Lamin (wa tatu kushoto) akimwakilisha Ann Therese Ndong’ Jatta, Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki akimkabidhi rasmi ripoti ya mradi wa kijiji cha kidigitali (Unesco-Samsung Digital Village) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka (wa tatu kulia) kwa ajili ya uendelezaji baada ya majaribio wakati wa hafla iliyofanyika katika kituo cha mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni cha jamii ya wamasai (Community Arts Space-CAS) kilichojengwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ushirikiano wa Unesco kwenye kijiji cha Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo Naibu Katibu Mkuu Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Avemaria Semakafu (waliosimama kwa nyuma), Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (kushoto), Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa wa UNESCO nchini Tanzania, Dkt. Moshi Kimizi (wa pili kushoto), Diwani wa kata ya Ololosokwan, Mh. Yannick Ndoinyo (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa  Kitongoji cha Ololosokwan, John Pyando (kulia).
 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Abdul Rahman Lamin wakati wa hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali wilayani Ngorongoro mkoani Arusha. Wengine meza kuu kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Emmanuel Sukums pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mh. Rashid Mfaume Taka.
 Baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
 Baadhi ya wazee wa kijiji cha Ololosokwan waliohudhuria hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Mrisho Gambo katika picha ya pamoja na wananchi, viongozi wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa walioshiriki mara baada ya hafla ya Unesco kukabidhi kijiji cha digitali cha Ololosokwan kwa serikali iliyofanyika katika kijiji cha Ololosokwan, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

No comments: