Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
NAIBU
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dk.Faustine Ndugulile amesema hairuhusiwi katika duka la dawa kuwa na
dirisha la ushauri kwani huo si utaratibu huku ikielezea sababu
zinazosababisha usugu wa dawa.
Dk.Faustine
Ndugulile amesema hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya
Famasi yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumzia
maduka ya dawa kuwa na dirisha kwa ajili ya kutoa ushauri, Dk.Ndugulile
amesema kisheria hairuhusiwi kwani kuna mgawawanyo wa majukumu.
"Kuna
baadhi ya maduka ya kuuza dawa wameweke na madirisha kwa ajili ya kutoa
ushauri.Hairuhusiwi na hivyo baraza la famasi linatakiwa kusimamia hili
kwa kuhakikisha hakuna duka la dawa ambalo limeweka dirisha la
ushauri,"amesema Dk.Ndugulile.
Akizungumzia
usugu wa dawa kwa mtumiaji, Dk.Ndugulile amefafanua zipo sababu nyingi
ikiwamo ya matumizi ya dawa yasiyo sahihi na ulaji holela wa dawa.Amefafanua
mbali ya kuwapo kwa sababu hizo kuna tafiti ambayo imebaini kuna
vimelea ambavyo ni sugu wa hali ya juu kwa dawa zote zilizopo duniani.
Wakati
huohuo Dk.Ndugulile ameliezea baraza la Famasi kuwa anao ushahidi wa
baadhi ya watalaam wa famasi si waaminifu kwani wamekuwa wakiiba dawa na
hivyo hao wachache kuharibu sifa ya famasi.
Ameliomba
baraza la famasi kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wanaokiuka
sheria za famasi kwani kukaa kimya kunatoa nafasi ya baadhi yao kukika
sheria zilizopo, hivyo wafuatilie.Hivyo
amesema wenye tabia hiyo ya kuiba dawa waache mara moja kwani Wizara
yao inafuatilia huku akielezea kwa sasa hakuna tatizo la uhaba wa dawa
kwani zipo za kutosha.
Kuhusu
kilele cha maadhimisho hayo, Dk.Ndugulile amesema anampongeza Msajili
wa Baraza la Famasi pamoja na timu yake kwa kuona umuhimu wa kuadaa
maadhimisho hayo.
Amesema
kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema hivi "Taaluma ya Famasi kuelekea
Tanzania yenye uchumi wa viwanda" ambapo amesisitiza kupitia kauli mbiu
hiyo wanataaluma wanaunga mkono nia ya dhati na juhudi za Serikali
chini ya Rais Dk.John Magufuli katika kuboresha huduma za afya kwa
wananchi ili kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda.
"Sina
shaka kuwa wanataaluma kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje
mtaweka mikakati thabiti kupitia viwanda vya dawa ambavyo matokeo yake
yataboresha uchumi wa nchi na kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi
imara,"amesema Dk.Ndugulile.
Kwa
upande wa Meya wa Jiji la Dar es Salam Isaya Mwita amesema anapongeza
na namna ambavyo baraza hilo limejipanga kuhakikisha wanatoa huduma bora
za famasi huku akitoa ombi kwa Serikali kuandaa mazingira ambayo
yatatoa nafasi kwa kuongezeka kwa viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini.
Wakati
huo huo Baraza la Famasi limetumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio na
changamoto huku pia wakielezea mikakati waliyonayo katika kuhakikisha
wanaboresha huduma za famasi nchini.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao
katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao
katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja
Baadhi ya Washiriki
Meya
wa jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita akizungumza katika madhimisho
ya wiki ya wafamasia Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Msajili
wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego akitoa maelezo kuhusu
maadhmisho ya wiki ya wafamasia yaliyofanyika jana Mnazi Mmoja
Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya
kulizindua wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika leo
jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi.
Elizabeth Shekirego Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed
Bakari
No comments:
Post a Comment