Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Mei 16,2018 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga. Mkuu huyo wa wilaya amekabidhi vitambulisho 12,918 kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa hiyo watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
“Hapa nchini, hili ni zoezi la kwanza la ugawaji vitambulisho kwa wananchi kwa kutumia ugawaji wa mkupuo,tunaanzia katika manispaa ya Shinyanga,nakabidhi rasmi vitambulisho hivi kwa maafisa watendaji wa kata ambao watagawa vitambulisho kwa wananchi”,alieleza Matiro.
Aidha aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na kugawa vitambulisho hivyo haraka huku akisisitiza kuwa vitambulisho hivyo havitolewi kwa ubaguzi bali kila mwananchi ana haki ya kupata.
“Zoezi kujiandikisha linaendelea katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lakini kwa upande wa manispaa ya Shinyanga tumemaliza zoezi la uandikishaji kinachoendelea sasa ni kugawa vitambulisho,hili ni zoezi endelevu wale ambao hawajiandikisha wafike katika ofisi za NIDA kujiandikisha ili wapate vitambulisho”,aliongeza Matiro.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau alisema tangu waanze zoezi la uandikishaji mwezi Septemba 2017 katika manispaa ya Shinyanga wamezalisha jumla ya vitambulisho 17,780 na tayari wameshagawa vitambulisho 3651 kwa watumishi wa umma na leo vitambulisho 12,918 kwa wananchi na zoezi la uandikishaji na ugawaji vitambulisho linaendelea.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa aliwasisitiza wananchi ambao bado hawajisajili waendelee kujisajili katika ofisi za Uhamiaji huku akiwataka kutoa ushirikiano kuwafichua watu wasiostahili kupata vitambulisho hivyo.
“Uzalishaji wa vitambulisho unaendelea na tunatarajia hadi mwezi Desemba mwaka huu kila mwanachi awe na kitambulisho,NIDA inaomba wananchi kufichua watu wasiotahili kupata vitambulisho hivi wakiwemo wahamiaji haramu”,aliongeza Kapesa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi aliwataka maafisa watendaji kutoendekeza urasimu katika ugawaji wa vitambulisho na hatarajii kusikia kitambulisho cha mwananchi kimepotea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiwasisitiza maafisa watendaji wa kata kuwa makini katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wananchi ili kuepuka changamoto inayoweza kujitokeza ya kupotea kwa vitambulisho.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisoma taarifa ya zoezi la uandikishaji na utoaji vitambulisho vya taifa katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji vitambulisho.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya vitambulisho 12,918 vilivyokabidhiwa kwa maafisa watendaji wa kata 17 za manispaa ya Shinyanga watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya wakati akizindua rasmi zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akionesha kitambulisho chake cha taifa baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa diwani wa kata ya Lubaga Mchungaji Obedi Jilala (CHADEMA).
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi Kitambulisho cha taifa diwani wa viti Maalum Manispaa ya Shinyanga Mariam Nyangaka (CCM).
Diwani wa kata ya Kizumbi,Reuben Kitinya akipokea kitambulisho cha taifa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikabidhi Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji wa kata ya Mwawaza,Nhiga Nhiga ili akavigawe kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikabidhi Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji wa kata ya Ndembezi,Felister Msemelwa ili akavigawe kwa wananchi wa kata hiyo.
Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisisitiza jambo wakati wa zoezi la ugawaji vitambulisho vya taifa kwa maafisa watendaji wa kata za manispaa ya Shinyanga.
Maafisa watendaji na madiwani wakiwa ukumbini.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment