NA WAMJW-DAR ES SALAAM
TAASISI
ya Mifupa nchini MOI sasa itafanya upasuaji wa mifupa kwa wagonjwa
wapatao 1000 kwa mwezi kutoka wagonjwa 500 mpaka 700 baada ya kupokea
msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake kutoka kwa Serikali ya
Kuwait .
Hayo
yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha
upasuaji na vifaa vyake vyenye thamani ya shilinigi milioni 186 leo
katika Taasisi ya mifupa MOI leo jijini Dar es salaam.
“Hii
ni faraja kubwa sana kwa Serikali kwani uboreshwaji wa huduma katika
hospitali zetu za kibingwa kubwa kama MOI itaweza kuhudumia wagonjwa
wengi Zaidi kutoka wagonjwa 700 kwa mwezi mpaka kufikia 1000 kwa mwezi”
alisema Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha
Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Kuwait
kupitia Balozi wake Jasem Al Najem kwa msaada huo kwani utaisaidia kwa
kiasi kikubwa MOI katika kuboresha utoaji huduma hasa katika fani ya
upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi hapa nchini.
Kwa
uapnde wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa kukamilika kwa vyumba hivi
viwili vya upasuaji, kutaiwezesha Taasisi ya MOI kuwa na jumla ya vyumba
vya upasuaji 8 kutoka 6 vilivyopo sasa na miongoni mwa vyumba hivi vya
upasuaji kimoja kitakuwa maalumu kwa ajili ya watoto tu.
“MOI
imeshatoa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa 1,670 ikiwemo upasuaji
mifupa (wagonjwa 1,228), kubadilisha nyonga (wagonjwa 84), kubadilisha
goti (wagonjwa 72), upasuaji wa uti wa mgongo (wagonjwa 109), ubongo
(wagonjwa 64), na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (wagonjwa
113” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha
Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuimarisha na kuboresha afya za
Watanzania jengo hilo pia litakuwa na vitanda 16 vya ICU (Intensive Care
Unit) na 16 vya HDU (High Dependency Unit), hivyo kuimarisha huduma za
tiba kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Naye
Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem amesema kuwa Nchi ya
Kuwait ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha Hospitali na Vituo vya
afya nchini Tanzania vinatoa huduma bora za Afya kwa kutumia Taaluma na
ujuzi wa kisasa ikiwemo vifaa na vifaa tiba .
“Serikali
ya Kuwait itakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Tanzania katika kuimarisha afya za wananchi kwa kuendelea
kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa,vifaa tiba na wataalamu wa afya
na kutochoka katika hilo” alisema Balozi Najem.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Bi. Zakia Mejhi amesema kuwa
Taasisi yake imeokoa Bilioni 3 za kufanyia upasuaji kwani kwa sasa
huduma hizo za kibingwa zinafanyika nchini kwa Shilingi Bilioni 12
kutoka Bilioni 15 za rufaa ya kwenda kutibiwa nje.
No comments:
Post a Comment