Friday, May 11, 2018

BALOZI SEIF ALI IDD AFUNGUA MKUTANO MKUU WA TAPSEA, ZANZIBAR LEO

 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akitoa hotuba yake katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja,  Zanzibar leo. 
 Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd wakati akitoa hotuba yake katika Ufunguzi wa Mkutano wao Mkuu, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatib Hassan akizungumza machache na kutoa salamu ya Mkoa wa kwa Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee na Wanawake - Zanzibar, Modlen Kastiko akizungumza na kuwahusia Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), katika Mkutano wao Mkuu, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Doroth Mwaluko akisisitiza jambo katika Mkutano Mkuu Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akihamasisha jambo kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu Chama hicho, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto) akimpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga, kwa hotuba yake aliyoisomba mbele ya Mkutano Mkuu Chama hicho, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Doroth Mwaluko na Kulia ni Katibu Mkuu wa TAPSEA, Festo Melikiory. 

 Burudani ya Ngoma ya Kidumbaki ikiendelea kutumbuza Ukumbini hapo.
 

 

 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA).

 Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akiteta jambo na Katibu Mkuu wake, Festo Melikiory, wakati wa Mkutano huo.
No comments: