Friday, May 11, 2018

MAPATO YA UTALII YAONGEZEKA HAPA NCHINI

Na Mahmoud Ahmad Dodoma

Imeelezwa kuwa Ukuaji wa sekta ya utalii hapa nchini, umedhihirika mapato yatokanayo na utalii kuongezaka kutoka Dola bilioni 1.7 mwaka 2012 hadi kufikia Dola bilioni 2.2 mwaka 2017. 

Ongezeko la mapato hayo ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii kutoka 1,077,058 mwaka 2012 hadi kufikia watalii 1,327,143 mwaka 2017. Ambapo Sekta ya utalii inachangia takriban asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni (foreign exchange earnings).

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkta Hamis Kigwangala wakati akifungua kongamano la kupitia rasimu ya sera ya Taifa ya utalii ya mwaka1999 linalofanyika jijini hapa na kuwashirikisha wadau wa sekta ya utalii nchini kutoka sekta binafsi na za umma.

Kigwangala amesema kuwa maboresho hayo yaende sambamba na mwendelezo wa mchakato wa kazi nzima ya kupitia Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 ambayo ni muhimu kwa mstakabali wa sekta ya utalii hapa nchini ambayo Kama ilivyoelezwa hapo awali, mojawapo ya dhumuni la msingi la hatua hiyo linalenga kuwa na Sera inayoendana na mabadiliko ya kiuchumi, mazingira, tecknolojia, kijamii na kisiasa yanayotokea ndani na nje ya nchi yetu ambayo yanagusa maendeleo ya sekta ya utalii nchini.

Amesema kuwa warsha imejumuisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Umma na Binafsi ambao kwa namna moja au nyingine huguswa au hushiriki katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Aidha, kama mnavyofahamu, utalii ni sekta mtambuka na ili kufanikisha ukuaji wake unahitajika ushirikiano thabiti baina ya wadau wote. Ushirikiano huu utaweza kuleta matokeo chanya iwapo kuna Sera madhubuti ambayo mchakato wake wa maandalizi umeshirikisha wadau kikamilifu.

“ Vilevile, nawashukuru wadau wa Sekta Binafsi kupitia Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT) kwa kuchangia sehemu ya gharama ya kazi hii hususan, kuwezesha warsha ya kukusanya maoni Kanda ya Kaskazini iliyofanyika Jijini Arusha. Hakika ushirikiano wa namna hii ndio utawezesha kuendeleza sekta ya Utalii na hata kuwezesha nchi yetu kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati kama ilivyobainishwa kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2025”. Alisema Kigwangala

Amesisitiza kuwa, Sera hii itakuwa ni nyenzo nyingine muhimu za kuitekeleza ambazo ni Mkakati wa utekelezaji wa Sera na Progamu ya Maendeleo ya Utalii nchini. Tayari Wizara imeanza maandalizi ya awali ya kukamilisha nyenzo hizo na kuwa watashirikishwa kikamilifu katika kuziandaa na kuitekeleza.

Nae katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja jenerali Gaudence Milanzi akimkaribisha mgeni rasmi amesema kuwa Mafanikio haya ya Sekta ya utalii yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 na juhudi za Serikali kutekeleza Sera hiyo kwa ushirikiano na Wadau katika usimamizi, uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za utalii, utangazaji katika masoko mbalimbali ya utalii duniani na mazingira bora ya uwekezaji na kuibuka na maboresho kwa ajili ya rasimu hii ya Sera kwa mustakabali wa sekta ya Utalii nchini.

Amesema kuwa lengo la kuhuisha rasimu ya serĂ¡ ya taifa ya utalii ni la wadau wote wa sekta hiyo hivyo serĂ¡ hiyo ilifanyiwa mabadiliko miaka 18 iliyopita na kuweza kuifikisha sekta hii hapa ilipo ni busara zetu sasa ziweze kutufikisha kufikia kwenye malengo tarajiwa kwa kuwashirikisha wadau wote katika mchakato mzima hili limepelekea leo kuja na rasimu hii.

No comments: