Saturday, April 28, 2018

Woolworths yafungua duka Mlimani City, yajipanga kufunga lingine Dodoma

Kampuni ya nguo la Woolworths imefungua duka mpya la nguo lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, likiwa ni duka la tano la kampuni hiyo kwa hapa nchini.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi huo, Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki alisema huo ni mwendelezo kampuni hiyo kufungua maduka ambayo yanauza nguo zenye viwango bora na hivyo kuwataka wananchi kutembelea maduka hayo ili kununua nguo.

Alisema baada ya ufunguzi wa duka hilo wamejipanga kufunga duka lingin makao makuu ya nchi Dodoma ili kuwasogezea bidhaa zao wateja wao na hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi wa serikali wamehamia mkoani humo.

"Ni hatua nzuri kwenda mbele, uchumi kwa sasa ni mgumu, wakati wengine wafunga maduka sisi tunafungua kubwa nchini kuliko yote, tumeweza kudhibiti mdororo wa uchumi pamoja na kuwa tumeshindwa kufikia malengo yetu lakini tumekuwa imara,

"Kuanzia mwaka kesho tutaanza kuangalia ujenzi wa duka Dodoma, Dodoma ni makao makuu ya nchi, wapo viongozi wa Serikali na hakuna huduma kama hizi. Tumeanza kuongea na wajenzi ili katika miaka miwili ijayo tufungue duka Dodoma," alisema Mafuruku.

Aidha alizungumza kuhusu wafanyabiasha ambao wanakwepa kodi ambapo kuhusu kampuni yao alisema wamekuwa wakilipa kodi zote ambazo wanatakiwa kulipa na kutumia nafasi hiyo kuwataka wanaokwepa kulipa kodi waache tabia hiyo.

"Mtu anayefanya biashara kwa kutokuwa mwaminfu ipo siku atapambana na serikali, ila sisi sitaki kusikia mfanyakazi anakuja kusema bosi hii pesa nimemhonga mtu wa TRA, sisi kila siku tunawafundisha wafanyakazi wetu walipe kodi zote, hata kama ni kubwa," alisema.
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akikata utepe kuashirikia ufunguzi wa duka duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Rabi Hume)
Mwenyekiti wa Woolworths Tanzania, Ali Mafuruki akiingia katika duka la nguo la Woolworths lililopo jijini Dar es Salaam. 

No comments: