Wednesday, April 18, 2018

Watanzania wahimizwa kujenga utamadunI wa kujisomea vitabu

Watanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuacha tabia ya  kutumia vitabu kama sehemu salama ya kuhifadhia fedha ,  kama ilivyo kwa baadhi ya watu maeneo ya vijijin na mjini  huku waandishi wa vitabu wakitakiwa kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga Taifa lenye wasomi.


Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, ambapo amesema  jamii nyingi za kitanzania zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa  na kuongeza maarifa baadala yake wanatumia  vitabu kama sehemu ya kuhifadhia fedha  jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa vitabu.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu Duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  prof,Ganka Nyamusogoro akikagua moja ya vitabu vilivyooneshwa na chuo cha mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu Duniani,ambapo chuo cha mzumbe kimetoa nafasi kwa watu mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu kwa siku tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
 Wanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe  mkoani Morogoro na shule ya sekondari Mzumbe wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi  katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho Prof, Ganka Nyamusongoro hayupo pichani.
 Diwani wa kata ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi wa kwanza kushoto  akisisitizia wanafunzi  juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
  Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro ambaye pia ni Mgeni rasimi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani chuo kikuu Mzumbe  Mkoani Morogoro  akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa na wanazuoni wa chuo kikuu cha mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.
 Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro Alfred  Joseph King akijisomea jarida wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu  duniani, jarida hilo  limechapishwa na chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro (katikati) akiangalia hotuba inayohusu maadhimisho ya siku ya vitabu  duniani ambapo kushoto kwake ni mkuu wa idara ya huduma za wasomaji chuo kikuu cha mzumbe Sarah Mwambalaswa na kulia ni Mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila .
Wa kwanza kushoto ni David Onyango mkutubi wa maktaba ya chuo kikuu cha mzumbe akimuonesha vitabu vilivyo pangwa katika maktaba maalumu ya madhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani,wa pili kushoto Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro anae fatia ni Diwani wa kata ya Mzumbe mkaoni Morogoro Recho Kungi wa mwisho ni  mkurugenzi maktaba na huduma za kiufundi chuo kikuu mzumbe Dk Arobogasti Musabila

No comments: