Wednesday, April 18, 2018

TAMASHA LA AMKA KIJANA, TUIJENGE IRINGA YETU LAFANA MJINI IRINGA

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akimtambulisha mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (mwenye ushungi) huku mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akifuatilia kwa karibu wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa Mwembetogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela (kushoto) akifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na msanii wa Muziki wa Singeli, Dulla Makabila wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda nae hakuwa nyuma kutoa burudani. Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akizungumza na wana-Iringa waliojitokeza katika amasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Msanii wa Bongo Movies, Steve Nyerere ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu akizungumza machache na wakazi wa Iringa juu ya kutunza Amani, Upendo na Mshikamano wetu katika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwatambulisha wasanii wa Bongo Movie waliofika katika Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Mratibu wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu, Msanii wa Bongo movies, Single Mtambalike (Rich Rich) akizungumza machache wakati wa tamasha hilo lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akieleza machache. Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB ' akimtambulisha msanii mwenzake Weru Sengo. Msanii wa Kundi la Ze Komed akitoa burudani. Mchekeshaji maarufu, Mama Asha Boko akitoa burudani. Dj Choka nae alipata wasaa wa kutoa neno kwa wana-Iringa. Msanii wa Bongo Movies, Anti Ezekiel akiwasalimu wakazi wa Iringa.
Msanii wa Bongo Movies, Jackline Wolper toa burudani.
Wanamuziki wa bendi ya Fm Academia Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani.
Wasanii wa Bongo movies wakipata picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na viongozi wengine wa Mkoa mara baada ya kumalizika kwa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu.

No comments: