Na Joel Maduka ,Chato
Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato.Ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.
Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara zao.
Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.
“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi wa Shirika la White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi 16 kwenye jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni Sh Bilioni 78.56.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.
Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.
Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.
Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani.
No comments:
Post a Comment